-
Welcome
-
UJENZI WA BARABARA MUHIMU AFRIKA MASHARIKI KUANZA
UJENZI wa awamu ya tatu ya kipande cha barabara kuunganisha nchi ya Tanzania na Kenya umezinduliwa.
-
RELI YA KASKAZINI KUTOKA TANGA HADI ARUSHA KUANZA KUTUMIKA MWEZI APRILI MWAKANI
Serikali imesema imeanza kufufua reli ya Kaskazini ya kutoka Tanga hadi Arusha ambayo ilikufa miaka 14 iliyopita ili kuwezesha wafanyabiashara na wananchi kusafirisha mizigo yao kwa kutumia reli hiyo badala ya barabara hali itakayopelekea kupunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara nchini.
Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokagua ukarabati wa reli hiyo kuanzia eneo la Korogwe hadi Mombo ambalo limekamilika kwa KM 83 na kuwahikikishia watanzania kuwa uendelezaji wa reli hiyo hadi Arusha itakamilika mapema mwezi Aprili mwakani na hivyo kuruhusu huduma za usafirishaji ziendelee hasa za mazao na bidhaa.
"Niwahakikishie wananchi kuwa hii kazi tuliyoianza haiwezi kusimama kwani Serikali imejipanga na itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri za usafirishaji", amesema Waziri Prof. Mbarawa.