-
Welcome
-
RAIS SAMIA HASSAN AHAHIDI KUKAMILIKA KWA MIRADI YA BARABARA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 17 Mei 2022 amefanya ufunguzi rasmi wa barabara ya Tabora-Nyahua-Chaya kipande cha Nyahua-Chaya (km 85.4) wilayani Uyui mkoani Tabora.
-
BARABARA YA TABORA HADI MPANDA YAKAMILIKA KWA KIWANGO CHA LAMI
Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 18 Mei 2022 amefanya ufunguzi rasmi wa barabara Tabora, Koga hadi Mpanda yenye kilomita 342.9 iliyo kamilika kwa kiwango cha lami inayounganisha mikoa wa Katavi na Tabora.
-
WAZIRI KAMWELWE AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA MAPEMA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amemtaka mkandarasi wa kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), anayejenga barabara ya Nyahua –Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kukamilisha barabara hiyo ifikapo mwezi Desemba 2020 badala ya Machi 2021.
-
TANROADS YATAKIWA KUILINDA MIUNDOMBINU YAKE
Kamati ya Bunge ya Miundo mbinu imeutaka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), kujipanga nakuja na mikakati bora ya kuilinda miundombinu ya barabara za lami inazozijenga hapa nchini ili ziwe fursa za kiuchumi badala ya kuwa chanzo cha ajali.
-
UJENZI WA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA KM 85.4 KWA KIWANGO CHA LAMI WAANZA RASMI.
Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kampuni ya CHICO kutoka China, ili kuweza kuufungua mkoa wa Tabora na mikoa jirani ya katavi na kigoma.
-
PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewataka makandarasi wazawa wa kampuni ya Samota, Anam na Jossam JV wanaojenga barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha lami wahakikishe wanakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliowekwa.
-
NAIBU WAZIRI KWANDIKWA: ZINGATIENI VIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA BARABARA
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ametoa wito kwa madiwani nchini kuanisha barabara zote zenye kipaumbele katika maeneo yao ili ziweze kuingizwa kwa urahisi kwenye mpango wa matengenezo.
Kwandikwa ametoa wito huo mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo yenye urefu wa KM 28 ambapo pamoja na mambo mengine amesema mapendekezo yao yawasilishwe katika kamati za maendeleo za wilaya, mikoa na bodi za barabara.
"Unakuta diwani analalamika kwamba barabara haijatengenezwa ama haifikiliwi kutengenezwa lakini ukija kufuatilia unakuta hakuna mahali popote ambapo taariza za barabara hiyo kutengenezwa zimewasilishwa", amesema Mhe. Kwandikwa.