• Welcome

 • SERIKALI IMEKAMILISHA MIRADI MIKUBWA YA BARABARA MKOANI SONGWE

  Serikali kupitia TANROADS Mkoani Songwe imekamilisha miradi mikubwa ya Kitaifa ya Barabara ikiwemo Daraja la Mto Momba ambalo limekuwa kiungo Muhimu kuunganisha Mikoa ya Songwe Rukwa na Katavi na barabara ya Mpemba hadi Isongole 50Km inayounganisha Tanzania, na Malawi.
  Akizungumza na Waandishi wa habari mara ya kutembelea miradi kadhaa Ofisini kwake mkoani Songwe Mei 03-2023 Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Songwe Eng. Suleiman Bishanga amesema kwa ujumla hali ya barabara zote ni nzuri na zote zinapitika katika kipindi chote cha mwaka.
  Amesema Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 11.29 katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023, kati ya fedha hizo shilingi bilioni 2.53, ni fedha za maendeleo, fedha ambazo zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali kuhakikisha barabara zote zinakaa vizuri.
  "Serikali imeupa kipaumbele miradi nane mkoani Songwe ambayo itaenda kukuza uchumi ukizingatia kuwa huu upo kwenye lango kuu la SADC, Uchumi, Magari, Mizigo inaingilia Songwe kuelekea Dar-es Salaam au kutoka Dar-es Salaam kwenda nchi Jirani za Zambia, Congo na kwenda SADC"
  Kaimu Meneja huyo wa TANROADS Songwe ametaja miradi kadhaa ya kipaumbele katika mkoa huo kuwa ni pamoja na barabara ya Tunduma kwenda Igawa Km 218 ambayo Serikali imepanga kuitengeneza kwa njia nne, Mlowo kwenda Kamsamba Km 130 yenye mchepuko wa kipande cha KM17.
  Barabara ya Mpemba-Isongole KM 50, Ruanda -Nyimbili- Hasamba -Izyila- Itumba- Mahenje na Hasamba, Vwawa Km 21 Isongole II - Kasumulo - Katumbasongwe KM 124 inayounganisha Songwe, Mbeya na Nchi jirani ya Malawi.
  Ameeleza miradi mingine ya barabara ya kipaumbele ni Chang'ombe - Patamela hadi Makongolosi wilayani Songwe ambayo itaunganisha mikoa ya Songwe Mbeya kuelekea Tabora na Singida pamoja na madaraja mawili ya Mto Muhesa na Maganga ambayo yatakuwa ufumbuzi wa kudumu kwa wananchi wa wa maeno hayo ambao ni wazalishaji mazao, Madini na Ufugaji.
  Ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kutengeneza kituo cha ukaguzi wa pamoja cha Iboya ambacho kitahusisha idara zote za serikali na kitakuwa na huduma zote za hoteli na maegesho ya magari.
  "Ili tuweze kukuza miji yetu, serikali imepanga kufanya mchepuo wa barabara kwa mjiji yetu, ambazo zitatusaidia katika mji wa Vwawa hadi Mpemba na mchepuko wa Tunduma hivyo mtu anayesafiri kwenda Rukwa hataitaji tena kwenda Tunduma atakatiza na kwenda kutokea mizani ya Mkangamo" ameeleza Mhandisi Bishanga.
  Aidha TANROADS mkoa wa Songwe inahudumia mtandao wa barabarani KM 982.6 kati ya hizo lami KM 255, 727 KM ni za changarawe, Madaraja jumla 224 kati hayo madaraja 75 yapo barabara kuu na barabara 149 yapo barabara za mkoa, hali ya barabara zote ni nzuri kwa 94%, 5% zipo hali ya wastani 1% zilikuwa hali mbaya lakini tayari hatua zimeshachukuliwa.

 • PROF. MBARAWA AMCHARUKIA MKANDARASI WA SIA

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa mkandarasi GM Construction anayejenga jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), kukamilisha ujenzi huo.