-
Welcome
-
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
-
MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kumuandikia barua mkandarasi wa Kampuni ya Impesa di Construzioni anayejenga kituo cha ukaguzi wa pamoja (one stop inspection station) eneo la Manyoni mkoani Singida na Nyakanazi mkoani Kagera kurejea eneo la kazi na kuendelea na ujenzi.
-
UJENZI WA KITUO CHA UKAGUZI WA PAMOJA MANYONI KUKAMILIKA SEPTEMBA MWAKA HUU
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja (One Stop Inspetion Station-Osis) kinachojengwa Wilayani Manyoni, Mkoani Singida na Kampuni ya Impresa di Costruczioni Ing. E. Mantovan S.p.a con socio unico Via Belgio ya nchini Italia na kusema kuwa kukamilika kwake kutarahisisha uchukuzi katika nchi za ukanda wa kati.
-
WASANIFU MIRADI YA UJENZI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ameyataka makampuni yanayopewa kazi na Serikali ya kusanifu ujenzi wa barabara kufanya kazi hiyo kwa umakini kwa kutambua na kubainisha changamoto zitakazosababisha ucheleweshaji wa ujenzi wa miundombinu hiyo hapa nchini.