• Welcome

 • SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAKAMILISHA UKARABATI WA UWANJA WA NDEGE WA MTWARA NA BARABARA YA LAMI KM 50 KUTOKA MTWARA HADI MNIVATA

  SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAKAMILISHA UKARABATI WA UWANJA WA NDEGE WA MTWARA NA BARABARA YA LAMI KM 50 KUTOKA MTWARA HADI MNIVATA

 • BILIONI 268 ZIMEELEKEZWA MTWARA KWENYE BARABARA, KUUFUNGUA MKOA WA MTWARA KIUCHUMI.

  Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent L. Bashungwa(Mb) amesema shilingi Bilioni 268 zimetengwa kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara - Newala Masasi (km 210); sehemu ya Mnivata - Newala - Masasi (km 160) kwa kiwango cha lami ili kuufungua mkoa wa Mtwara kiuchumi, kijamii na kuchochea biashara katika ukanda huo wa Mikoa ya Kusini.

 • WANANCHI WA MTWARA KUONDOLEWA KERO YA USAFIRI

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia TANROADS imesaini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Mnivata – Newala – Masasi (km 160) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa daraja la Mwiti lengo likiwa ni kuwaondolea wananchi kero ya usafiri wa barabarani na kuboresha mtandao wa barabara na madaraja ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji, hivyo kukuza uchumi wa nchi.

 • TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazokwamisha mradi wa ujenzi wa gati mpya.

  Prof. Marawa ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Gati mpya inayojengwa Mkoani Mtwara kwa ubia wa kampuni mbili za Kichina za China Railways Major Bridges Engineering Group Co. Ltd (CRMBEG) na China Railways Construction Engineering Group (CRCEG) na kubaini mapungufu katika utekelezaji wa mradi huo.

  “Hatuwezi kuendelea kuchelewesha mradi huu muhimu kwa wakazi wa Mtwara, wakati fedha zipo na mikataba imeshasainiwa, naiagiza TPA kuhakikisha kuwa inatatua changamoto hizo na kuzitafutia ufumbuzi ndani ya miezi mitatu ili mradi ukamilike kwa wakati,” amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa na Wakandarasi wazawa chini ya usimamizi wa TPA isimamiwe kwa kuzingatia viwango na muda uliopangwa na kuahidi kurejea baada ya miezi mitatu kukagua maendeleo ya miradi hiyo.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka amemuhakikishia Prof. Mbarawa kuwa TPA itasimamia kwa karibu mradi huo na kuhakikisha mapungufu yote yanafanyiwa kazi kwa wakati.

  “Nipende kukuhakikishia Waziri kuwa  TPA tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo na kuanzia wiki ijayo tutaongeza kasi ya kutatua mapungufu yaliyopo ili mradi huu ukamilike kwa wakati,” amesema Mhandisi Mattaka.

  Kwa upande wake Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali amesema kuwa kwa sasa mradi wa ujenzi wa gati namba mbili (2) umefikia asimilia 15 na utakapokamilika utawezesha Meli kubwa na za kisasa aina ya Panamax kuhudumiwa katika Bandari ya Mtwara ifikapo mwaka 2019.

  Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amekagua ujenzi wa Barabara ya Mtwara hadi Mnivata KM 50 na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo na kuahidi kulipa madai ya Mkandarasi Kampuni ya M/s Dott Services ltd mapema iwezekanavyo ili mradi huo ukamilike kwa wakati.

  ‘Nimhakikishie Mkandarasi kuwa madai yake aliyowasilisha tunajipanga kuyalipa ili kasi iwe kubwa na mradi huu ukamilike kwa wakati kwa kuwa umesubiriwa na wananchi wa mkoa wa Mtwara kwa muda mrefu’ Amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Aidha, Mkandarsi wa Kampuni ya M/s Dott Services ltd amemhakikishia mhe. Waziri  kuwa watahakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na kwa viwango kama ilivyoahidiwa.
  Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) , Mkoani Mtwara, Eng. Dotto John ametanabahisha kuwa wakala umejipanga kuhakikisha unasimamia barabara hiyo kwa kuhakikisha viwango na ubora vinazingatiwa na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

  Prof. Mbarawa yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya miradi ya Miundombinu ya Barabara na Bandari.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

 • KWANDIKWA AWATAKA ‘TAA NA TPDC’ KUHAMISHA BOMBA LA GESI UWANJA WA NDEGE MTWARA

  Naibu Waziri wa ujenzi, Elias Kwandikwa, ameiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kulihamisha bomba la gesi lililopitishwa katika maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kabla ya bomba hilo halijaleta madhara kwa watumiaji wa Uwanja huo.

 • TBA YATAKIWA KUHAKIKISHA MAENEO YAO YANA HATI.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ametoa agizo kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha wanazitambua na kuzisajili nyumba zote na viwanja vya Serikali zinazomilikiwa na Wakala huo katika maeneo mbalimbali nchini.

 • SERIKALI YAMCHARUKIA MKANDARASI DOTT

  Serikali imemtaka Mkandarasi Dott Services anayejenga barabara ya Mtwara-Mnivata yenye urefu wa KM 50 kwa kiwango cha lami kuongeza vifaa na kasi katika ujenzi wa barabara hiyo ili kurahisisha huduma za usafirishaji wa mazao na abiria kwa wananchi wa mkoa huo.