-
Welcome
-
Mafunzo maalum yaliyolenga Uzingatiaji Sheria, Kanuni, Taratibu katika Utendaji wao wa kazi hususan katika Masuala ya Nidhamu
Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania wameshiriki Mafunzo maalum yaliyolenga Uzingatiaji Sheria, Kanuni, Taratibu katika Utendaji wao wa kazi hususan katika Masuala ya Nidhamu na kufanyika katika Ukumbi wa TAFORI, Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia Januari 28 hadi 29 yaliandaliwa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Miongoni mwa Washiriki wa Mafunzo hayo ni Mameneja wa Mikoa, Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Uhasibu na Utawala pamoja na Wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi (TAMICO) wa Makao Makuu na Mikoa.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uendeshaji Bwana Hija Ally Malamla. -
WANAWAKE WAASWA KUCHANGAMKIA KAZI ZA BARABARA
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema itahakikisha wanawake walio katika Sekta ya Uhandisi na Ukandarasi wanapata fursa za kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na matengenezo ya barabara.
-
WANAWAKE KUPEWA KIPAUMBELE MIRADI YA UJENZI
WANAWAKE KUPEWA KIPAUMBELE MIRADI YA UJENZI
-
UJENZI WA BARABARA YA KIDATU-IFAKARA KUKUZA UCHUMI WA MOROGORO
Serikali imesema imeanza ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara yenye urefu wa KM 66.9 kwa kiwango cha lami ambapo kukamilika kwake kutachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika wilaya za mkoa wa Morogoro.