• Welcome

  • TANROADS MANYARA YATOA ELIMU JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA HIFADHI YA BARABARA PAMOJA NA KUJIEPUSHA NA UVAMIZI  

    TANROADS MANYARA YATOA ELIMU JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA HIFADHI YA BARABARA PAMOJA NA KUJIEPUSHA NA UVAMIZI

  • TANROADS MANYARA YAANZA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA WAZIRI BASHUNGWA ENEO LA KATESH

    TANROADS MANYARA YAANZA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA WAZIRI BASHUNGWA ENEO LA KATESH

  • TANROADS MANYARA YAENDELEA NA KAZI YA MATENGENEZO YA BARABARA YA NGARENARO-MBULU

    TANROADS MANYARA YAENDELEA NA KAZI YA MATENGENEZO YA BARABARA YA NGARENARO-MBULU

  • KAZI YA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA YA KIBAYA – KIBERASHI INAENDELEA

    KAZI YA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA YA KIBAYA – KIBERASHI INAENDELEA

  • TANROADS MANYARA YAENDELEA NA KAZI YA MATENGENEZO YA DARAJA LA RUKETO BARABARA YA LOSINTAI - NJORO

    TANROADS MANYARA YAENDELEA NA KAZI YA MATENGENEZO YA DARAJA LA RUKETO BARABARA YA LOSINTAI - NJORO

  • TANROADS INAENDELEA NA MATENGENEZO KATIKA ENEO LA MBIGIRI WILAYANI KITETO LILILOATHIRIWA NA MVUA

    TANROADS INAENDELEA NA MATENGENEZO KATIKA ENEO LA MBIGIRI WILAYANI KITETO LILILOATHIRIWA NA MVUA

  • TANROADS YAKAMILISHA UJENZI WA NJIA MBADALA ENEO LA DARAJA LA MTO LOSINYAI MKOANI MANYARA LILILOHARIBIWA NA MAFURIKI YA MAJI YA MVUA

    TANROADS YAKAMILISHA UJENZI WA NJIA MBADALA ENEO LA DARAJA LA MTO LOSINYAI MKOANI MANYARA LILILOHARIBIWA NA MAFURIKI YA MAJI YA MVUA

  • RAIS SAMIA ASIKIA SAUTI YA WANANCHI WA DAREDA- MANYARA

    RAIS SAMIA ASIKIA SAUTI YA WANANCHI WA DAREDA- MANYARA

    Manyara

  • Rais Dkt. Samia adhamiria kuufungua kiuchumi mkoa wa Manyara kwa ujenzi wa barabara za lami

    Rais Dkt. Samia adhamiria kuufungua kiuchumi mkoa wa Manyara kwa ujenzi wa barabara za lami

  • MRADI WA KARATU HADI MASWA WA EPC+ FINANCING

    Serikali imeanza mchakato wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Karatu - Mbulu - Hydom - Sibiti River - Lalago - Maswa yenye urefu wa Kilometa 339 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 553.493.

  • BARABARA YA LABBAY HADI HAYDOM KUUNGANISHA ZAIDI MANYARA NA MIKOA YA JIRANI

    Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania [TANROADS] inatarajia kujenga kwa kiwango cha lami miradi mitatu mikubwa ya barabara ambayo itaunganisha mkoa wa Manyara na mikoa ya Jirani.
    Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema hayo leo tarehe 19 mei -2023 mji mdogo wa Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara kwenye utiaji saini wa ujenzi wa barabara ya lami ya km 25 kutoka Labbay hadi Haydom.
    Ametaja miradi ya barabara ambayo imepangwa kutekelezwa na bajeti ya mwaka 2023/2024 inayotarajia kusomwa Bungeni Jumatatu ya Tarehe 22 Mei -2023 ni pamoja na km 389 za lami kutoka Karatu Mkoani Arusha, kwenda Mbulu na Haydom mkoani Manyara, Sibiti, Lalago- Maswa mkoani Simiyu.
    Mhandisi Kasekenya ameongeza kuwa Mradi wa pili wa barabara utakaojengwa ni km 424 kutoka Kiberash wilayani Handeni mkoani Tanga, kupitia Kibaya mkoani Manyara, Goima, Chemba, Dosee, Farkwa, Kwa Mtoro, mkoani Dodoma hadi mkoani Singida na tatu ni km 430 kutoka Kongwa mkoani Dodoma, Kibaya wilayani Kiteto, Losinyai wilayani Simanjiro mkoani Manyara hadi Mbuda mkoani Arusha.
    Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng: Rogatus Mativila akitoa taarifa fupi wakati wa kutia saini mkataba na Kampuni ya JIANGXI GEO –ENGINEERING GROUP LIMITED kwa ajili ujenzi wa barabara ya lami ya km 25 kutoka Labbay hadi Haydom unaogharimu shilingi bilioni 42.271 amesema kilomita hizo 25 zinakamilisha kilomita 50 kati ya kilomita 113 za barabara ya Serengeti Southern bypass zilizopo ndani ya mkoa wa Manyara.
    Eng: Mativila ameongeza "Nitoe Shukrani za dhati kwa Serikali yetu kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huu, Wakala ya Barabara (TANROADS) itasimamia utekelezaji wa mradi huu na kuhakikisha kuwa Mkandarasi anazingatia viwango vya kiufundi (Technical Standards) na mradi unakamilika kwa wakati, nitoe wito kwa Mkandarasi kufanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu ili kazi zote zikamilike ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango na gharama zilizokubalika"

  • BARABARA YA MBULU - HYDOM KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI - NAIBU WAZIRI UJENZI NA UCHUKUZI

    BARABARA YA MBULU- HYDOM KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI-  NAIBU WAZIRI  UJENZ INA UCHUKUZI

    Na Mwandishi wetu.

    Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya amesema barabara ya Mbulu-Hydom yenye urefu wa kilomita 70.5 ni sehemu ya barabara ya Karatu, Mbulu-Hydom, Sibiti, Lalago, Maswa zenye urefu wa kilomita 398 zinahudumiwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).

    Mhandisi Kasekenya ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Mjini, Zacharia Paul Isaay lBungeni jijini Dodoma kuhusu ujenzi wa barabara  ya Mbulu-Hydom,   amesema kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa barabara hiyo kupitia mradi wa Serengeti (Southern Bypass), ili kuijenga kwa kiwango cha lami umekamilika.

    Naibu Waziri amesema kazi hiyo imefanywa na kampuni ya HB Golf Engineer na KGGB zote za Ujerumani mwaka 2016 kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW).

    Amesema kwa kuzingatia umuhimu wa barabara hiyo, Serikali ilianza kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya Mbulu-Hydom yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami, ambapo katika mwaka wa fedha 2019/2020 ilitenga shilingi bilioni 1.45 na mwaka huu wa fedha imetenga shilingi bilioni 5.

    Naibu Waziri amesema ujenzi wa barabara hiyo utatekelezwa kwa njia ya kisanifu na zabuni ya kazi hiyo itatangazwa wakati wowote katika wakati huu wa mwaka wa fedha.

    Katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, zimetengwa shilingi milioni 401 kwa ajili ya kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hiyo ili iendelee kupitika katika majira yote ya mwaka huu.

  • BARABARA YA SIMIYU - MBULU HADI ARUSHA KUJENGWA KWA LAMI

    Serikali imeanza usanifu kwa ajili ya ujenzi  wa barabara ya lami itayounganisha Mikoa ya Simiyu, Singida, Manyara na Arusha ili kupunguza umbali wa safari uliopo sasa.