• Welcome

  • GATI YA LINDI YAKAMILIKA

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA) kwa kukamilisha ujenzi wa gati ya Lindi na kuwataka kutafuta masoko ili bandari hiyo iweze kunufaisha Serikali na wananchi wa Mkoa huo.

    Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo mkoani Lindi ambapo amesema mradi umekamilika kwa asilimia 92 na kukamilika kwa gati hiyo kutarahisisha biashara na kukuza uchumi kwa wananchi kwani meli kubwa zitaanza kutia nanga katika bandari hiyo.

    “Napenda kuwapongeza sana TPA kwa kazi kubwa mliyoifanya kukamilisha mradi huu, ni wakati sasa mkatafute masoko ili mpate faida na kurahisisha usafirishaji kati ya mkoa huu na visiwa vinavyozunguka” amesema Prof. Mbarawa.

    Waziri Prof. Mbarawa ameongeza kuwa pamoja na kukamilisha mradi huo TPA itunze miundombinu hiyo na kuifanyia ukarabati wa mara kwa mara ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

    Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka, amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa, kuwa Mamlaka itazingatia maelekezo yake na kuahidi kusimamia sehemu ndogo iliyobaki ili iweze kukamilika kwa wakati na viwango vilivyokubaliwa.

    Mhandisi Mattaka ameongeza kuwa ujenzi wa gati hiyo imegharimu kiasi cha shilingi zaidi ya bilioni 3 na fedha hizo zimefadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Katika hatua nyingine Waziri Profesa Mbarawa, amesema Kivuko kwa ajili ya Lindi na Kitunda kitawasili mapema katikati ya wiki ili kianze kutoa huduma kwa wakazi wa mkoa huo.

    Aidha ameauagiza uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kuhakikisha wanatafuta fedha na kujenga majengo ya abiria kwa upande wa Lindi na Kitunda ili kupunguza changamoto inayowakabilia abiria hasa nyakati za mvua.

  • NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA TEMESA KUPELEKA KIVUKO LINDI

    Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ameuagiza Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) makao makuu kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko kipya  kutoka eneo kinapotengenezwa wilayani Pangani mkoani Tanga hadi mkoani Lindi.

  • WANANCHI WA LIWALE NA NACHINGWEA WALILIA BARABARA

    Wananchi wa wilaya ya Liwale na Nachingwea mkoani Lindi wameiomba Serikali kuhakikisha inaanza ujenzi wa barabara ya Liwale - Nachingwea (Km 129) kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafirishaji wa abiria na mazao katika wilaya hizo.