• Welcome

 • NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWAPONGEZA TANROADS KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), amewapongeza Wakala wa barabara nchini (TANROADS), kwa mikakati wanayotumia kudhibiti vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini.

 • KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ametoa muda wa siku 21 kwa Mkandarasi Nyanza Road Works kuongeza vifaa vya kazi na wafanyakazi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

 • KWANDIKWA: ACHENI VITENDO VYA HUJUMA MIRADI YA UJENZI

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (Mb), amewataka wananchi wanaopata nafasi za kazi katika miradi ya ujenzi wa barabara kuwa wazalendo katika kulinda vifaa na kuepuka vitendo vya hujuma vinavyoweza kujitokeza ili kuhakikisha miradi hiyo inaenda kwa kasi na kumalizika kwa muda uliopangwa.

  Mhe. Kwandikwa ametoa kauli hiyo wilayani Kasulu mkoani Kigoma, alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 inayojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation na kuelezwa kuwa kuna wizi wa mafuta kiasi cha lita elfu 23 zilizoibiwa hivi karibun ambapo amewataka wananchi kuwa na uzalendo kwanza katika miradi yote ya ujenzi katika maeneo yote.

  "Wizi wa namna hii haukubaliki na mtandao ni mkubwa hivyo naagiza vyombo vya usalama vichukue hatua kali mapema ili kuweza kuondoa madhara makubwa zaidi", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

  Amewataka makandarasi na wasimamizi wa miradi kutoa elimu kwa waajiriwa kila siku kabla ya kuanza kazi kukemea tabia za wizi na ubadhilifu wowote utakaowezea kutokea kwani ni moja ya sababu za miradi pia kuchelewa na gharama kuongezeka.