• Welcome

 • MIKAKATI YA RAIS SAMIA KUINUA MAKANDARASI WAZAWA.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, anataka kuona ushiriki mkubwa zaidi wa Makandarasi wazawa katika kazi za utekelezaji wa ujenzi wa miradi nchini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa leo tarehe 21 Novemba, 2023 katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Makandarasi wazawa na Washauri elekezi wa ndani jijijini Dodoma, kujadili nafasi yao katika utekelezaji wa miradi.

  Bashungwa amesema Wizara ya Ujenzi, kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), inaendelea kutenga miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kwa ajili ya Makandarasi wa ndani kwa lengo la kuwasaidia Makandarasi hao kukua na kupata uzoefu.

  "Katika mwaka wa fedha 2023/204, jumla ya miradi minne ya barabara yenye urefu wa kilometa 50 kila moja zimetengwa kwa ajili ya makandarasi wa ndani tu, kwa hiyo kilometa 200 zitajengwa na wazawa, hii ni fursa kubwa ya kuwasaidia makadarasi", amesema Bashungwa.

  Aidha, Bashungwa amesisitiza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 Jumla ya kilometa 20 za barabara zimetengwa kwa ajili ya makandarasi wanawake, ambapo zitagawanywa katika vipande vya kilometa tano tano, na kazi hizo zitashindanishwa kwa makampuni ya wanawake peke yao, hii inafanya jumla ya km 220 kujengwa na makandarasi wazawa kwa mwaka 2023/24.

 • WAZIRI BASHUNGWA AWAFUNDA MAMENEJA TANROADS, ASISITIZA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.

  Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amewataka Mameneja wa Mikoa wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kuhakikisha wanaendelea na mapambanona dhidi ya rushwa katika maeneo yao ya kazi na nje ya kazi ili kujenga taswira nzuri kwa Wakala huo na Taifa kwa ujumla.

 • WAZIRI WA UJENZI MHE. BASHUNGWA AZINDUA BODI YA USHAURI YA TANROADS

  Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ameitaka Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuandaa mkakati utakaowawezesha na kuwasaidia Wakandarasi Wazawa kukua na kutekeleza miradi mikubwa kama ambayo inatekelezwa na Wakandarasi wa Nje ili fedha watakayolipwa ibaki hapa Nchini kukuza uchumi wa Nchi yetu.

 • TANROADS IMEJIPANGA VIZURI KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA EPC + FINANCING

  Meneja wa Miradi ya Public Private Partinerships- PPP na Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC +F) Mhandisi Harold Kitainda amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imejipanga kikamilifu kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya barabara za lami zenye jumla ya kilometa 2,035 zinazojengwa kwa wakati mmoja hapa Nchini kwa kutumia utaratibu mpya wa EPC + F ikiwemo mradi wa kilometa 384 kutoka Handeni mpaka Singida.

 • TANROADS YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU UBORA WA VIFAA KATIKA MIRADI

  Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), umewatoa hofu Watanzania kuhusu ubora wa vifaa vinavyotumika katika utekelezaji wa miradi inayoendelea nchini ikisema ni imara na bora.

 • SERIKALI IMESAINI MIKATABA MIKUBWA 7 KWA UTARATIBU WA EPC+FINANCING

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TANROADS imesaini mikataba mikubwa ya kujenga kwa kiwango cha lami Barabara 7 zenye jumla ya km 2,035 kwa kutumia Utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F),

 • MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI KATIKA UJENZI WA MIUNDOMBINU NCHINI

  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi Trilioni 3.554, katika mwaka wa fedha 2023/2024, kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni 1.468. ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi na Shilingi Trilioni 2.086, ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi.
  Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameomba fedha hizo mapema leo Tarehe 22 Mei -2022 wakati akisoma Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma.
  Kuhusu Miundombinu Waziri Prof. Mbarawa amesema serikali kupitia TANROADS inatarajia kuanza ujenzi wa miradi saba (7) ya barabara yenye jumla ya kilometa 2,035 kwa kutumia utaratibu wa Engineeering Procurement Construction and Finance ( EPC + F) na kuanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara kutoka Kibaha – Chalinze – Morogoro Expressway yenye urefu wa kilometa 205 kwa kutumia utaratibu wa kushirikisha Sekta Binafsi (Public Private Partnership – PPP.
  Amesema pia unaendelea na ujenzi wa miradi mikubwa ya barabara katika maeneo mbalimbali yenye jumla ya urefu wa kilometa 1,031.98 na Ujenzi wa Barabara iliyosaniwa Katika Mwaka wa Fedha 2022/23 yenye jumla ya urefu wa kilometa 393.6
  Amesisitiza kuwa miradi yote ya barabara na madaraja ikamilika itakuwa na jumla ya km 3,934.7 za barabara zilizojengwa kwa lami ambazo zitaongeza urefu wa mtandao wa barabara za lami zilizopo sasa za km 11,587.82 na kufikia km 15,522.52 ambalo ni sawa na ongezeko la 34%.
  Waziri Prof. Mbarawa ameongeza kuwa Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato Dodoma pamoja na Kuendelea na kazi za ukarabati na upanuzi wa viwanja vingine vya ndege katika mikoa mbalimbali ikiwemo Kiwanja cha Ndege cha Songwe, ukarabati na upanuzi wa Viwanja vya Ndege vya Sumbawanga, Shinyanga, Tabora na Kigoma.

 • FIDIA YA WANANCHI WA DODOMA JIJI WANAOPISHA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE MSALATO NA BARABARA YA MZUNGUKO

  Fidia ya wananchi wa maeneo wanaopisha ujenzi wa kiwanja cha kimataifa cha Ndege cha Msalato na Barabara ya mzunguko imekamilika na itaanza kutolewa ndani ya muda wa wiki mbili zijazo.

 • WAZIRI ISACK KAMWELWE AWASILI OFISINI JIJINI DODOMA LEO

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amewasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara yake mjini Dodoma leo na kulakiwa na watumishi wa Sekta hizo.

 • SHERIA MPYA KUDHIBITI UZITO KUANZA MWAKANI

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameitaka kurugenzi ya Usalama na Mazingira katika wizara hiyo kutoa elimu kuhusu kuanza kutumika kwa sheria mpya ya udhibiti wa uzito wa magari ya jumuiya ya afrika ya Mashariki ya mwaka 2016.

 • WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KUSHUGHULIKIWA

  Serikali imesema haitamvumilia mwananchi yoyote atakaebainika
  kununua vyuma vyenye alama za barabara kama chuma chakavu, ili iwe fundisho kwa wahujumu wa miundombinu ya barabara.

 • SERA MPYA YA UJENZI KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI

  SERIKALI imesema mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Ubungo hadi Kibaha Mkoani Pwani yenye urefu wa kilometa 16 unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu utasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa katika nchi jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.