• Welcome

 • WAZIRI MBARAWA ARUHUSU MAGARI KUPITA BARABARA YA JUU CHAN'GOMBE

  WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa leo ameruhusu kuanza kutumika kwa njia moja ya barabara ya Juu Chang'ombe ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza kabla ya kuanza kutumika kwa barabara hiyo, Prof. Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani kuhakikisha magari yanayotumia njia hiyo kwa sasa yanazingatia sheria za mwendo kwani bado ujenzi unaendelea eneo hilo.

  Alisema kutumika kwa barabara hiyo kutasaidia kupunguza msongamano hivyo, kuwasaidia watumiaji  wa barabara hiyo wapate muda wa kutosha kufanya shughuli zao kwani msongamano  katika eneo hilo unawapotezea muda.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mativila amemhakikishia  Mhe. Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni Awamu ya Pili ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa haraka BRT2 utakamilika  kwa ubora na kwa wakati.

  Eng. Mativila  amesema  ujenzi wote wa Barabara za Juu za Chang'ombe na Chuo cha Uhasibu unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

 • GARI KUANZA KUPITA UPANDE MMOJA BARABARA YA JUU UHASIBU, CHANG'OMBE.

  Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa wakati ujenzi barabara za juu eneo la Uhasibu na Chang’ombe ukiwa unaendelea gari zitaruhusiwa kupita upande mmoja wa barabara kuanzia Mei 30, mwaka huu. 

 • DARAJA LA TANZANITE INAVYOTATUA MSONGAMANO DAR ES SALAAM

  RAIS Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali

 • RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ARIDHISHWA NA UJENZI WA DARAJA JIPYA LA SELANDER

  Rais Samia Suluhu Hassan ameridhishwa na teknologia iliyotumika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi na kupanda kwa kina cha bahari katika kingo za Daraja jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030.

 • WAZIRI KAMWELWE ATOA SIKU SABA KWA MHANDISI MSHAURI KUPELEKA KAZI TANROADS

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, atoa siku saba kwa mhandisi mshauri kutoka kampuni ya Studi International aliyefanya usanifu wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato mjini Dodoma,  kukabidhi nyaraka za usanifu huo kwa Wakala wa Barabara (TANROADS).

 • PROFESA MBARAWA: MRADI WA UJENZI UBUNGO- KIBAHA KUIPAISHA NCHI KIUCHUMI

  SERIKALI imesema mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Ubungo hadi Kibaha Mkoani Pwani yenye urefu wa kilometa 16 unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu utasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa katika nchi jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.

 • BARABARA YA KIMARA BARUTI-CHUO KIKUU KUKAMILIKA NDANI YA SIKU 60

  Serikali imetoa siku 60 kwa mkandarasi wa Kampuni ya Hari Singh & Sons kumaliza ujenzi wa kipande cha barabara cha kilomita 1.5 kilichobaki kwa kiwango cha lami katika barabara ya Kimara Baruti-Msewe-Chuo Kikuu yenye jumla ya urefu wa kilomita 2.6.

 • Ujenzi wa Interchange kwenye makutano ya Ubungo

  Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), leo umetiliana saini na kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) mkataba wa ujenzi wa barabara za Juu ‘Interchange’ katika makutano ya barabara ya Sam Najoma na Mandela Ubungo jijini Dar es salaam.