• Welcome

  The TANROADS Regional Manager's office (RMO) for Arusha region is dedicated to manage the road network under its mandate, which extend throughout all six (6) districts. The trunk roads, traverse five (5) of these districts, namely Arumeru, Arusha, Monduli, Longido and Karatu. These districts are also networked with regional roads that extend into the sixth and remotest district of Ngorongoro.

  Apart from being under the Chief Executive of TANROADS the annual plans and performance reports of the RMO are subject to the review and advise of the Regional Roads Board (RRB). The RRB is chaired by the Regional Commissioner, and its Secretary is the Regional Administrative Secretary. The RRB membership comprises of Members of Parliament, at most three Members from the Private Sector, District Commissioners, the Mayor of Arusha City Council and Chairmen of District Councils, the Arusha City Director and District Executive Directors, TANROADS Regional Manager, Regional Secretariat Engineer and the Engineers in the City /District Councils. Sections 6 and 7 of the Roads Act, 2007 (Act No.13 of 2007) provide for the establishment, functions, composition, tenure and proceedings of the RRB.

 • Mhe. Rais Dkt Samia afanya makubwa utekelezaji wa miradi ya miundombinu Arusha

  Mhe. Rais Dkt Samia afanya makubwa utekelezaji wa miradi ya miundombinu Arusha

 • MTENDAJI MKUU TANROADS ATOA MAELEKEZO UTEKELEZAJI MIRADI YA EPC+ F

  Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania Mhandisi Mohamed Besta amesema TANROADS imepita katika vipindi tofauti lakini sasa ipo katika kipindi ambacho inabidi iwe na ubunifu wa kutumia mbinu mbalimbali na kutafuta namna bora zaidi ya kujenga barabara, na moja ya hatua ambazo zimechukuliwa na kuwekewa mkazo na Serikali ni pamoja na kutumia utaratibu wa EPC + F ili kujenga miundombinu hiyo kwa haraka zaidi.

 • MAKAMU WA RAIS AFUNGUA BARABARA YA LOLIONDO - MTO WA MBU

  Makamu wa Rais Dkt Phillip Isdor Mpango amefungua Barabara ya Loliondo–Mto Wa Mbu (km 217) Sehemu ya Wasso-Sale (km 49) ambayo imekamilishwa na Serikali kupitia TANROADS kwa kiwango cha lami wilayani Loliondo mkoani Arusha.
  Akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhudia barabara hiyo ikifunguliwa, leo tarehe 17 Mei 2023 Makamu wa Rais Dkt Mpango amesema pamoja na kwamba gharama za ujenzi wa barabara ni kubwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan itahakikisha inajenga kipande kilichobaki kwenda Mto wa Mbu.
  Kwa kuanzia Makamu wa Rais Dkt Mpango ameiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha kuwa inaweka kwenye Bajeti ya wizara hiyo itakayosomwa Jumatatu Mei, 22-2023 na kuomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa kipande kingine korofi cha barabara km 24 kutoka Ngaresero kwenda Engaruka wakati Serikali kupitia TANROADS ikiendelea na mchakato wa Ujenzi wa sehemu nyingine ya barabara hiyo.
  Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Geoffrey M Kasekenya amesema barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wa mkoa wa Arusha, wilaya ya Ngorongoro, Loliondo na vijiji vyote ambavyo barabara hiyo inapita na kwamba inahitajika sana na watalii wanaokwenda Mbuga ya Serengeti, lengo likiwa ni hadi kufikia mwaka 2025 mikoa yote iwe imeunganishwa na barabara nzuri kwa kiwango cha lami.
  "Naomba niwape Wananchi hawa Taarifa, Rais ametoa maelekezo, kipande cha km 10 kutoka Wasso kwenda Makao makuu Loliondo nacho kipo kwenye hatua ya manunuzi ili kijengwe kwa kiwango cha lami, Mtu akitoka makao makuu ya wilaya anakuja Wasso anaendelea na lami" ameongeza Naibu Waziri Kasekenya
  Akitoa taarifa fupi ya Mradi huo Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng: Rogatus Mativila amesema Ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha mtandao wa barabara nchini kwa kujenga Barabara Kuu na za Mikoa kwa kiwango cha lami.

 • BARABARA YA MCHEPUKO WA KUSINI (ARUSHA BYPASS) ARUSHA HADI KENYA KM 42.4 YAFUNGULIWA RASMI.

  Leo tarehe 21 julai 2022 kumefanyika ufunguzi rasmi wa Barabara ya mchepuo ya Arusha (Arusha Bypass) yenye urefu wa km 42.4. Uzinduzi huo uliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mwenzake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huku ukihudhuriwa pia na wakuu wa nchi na serikali wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, viongozi wa Jamhuri ya Sudan pamoja na Somalia.

 • KUITWA KWENYE USAILI

  KUITWA KWENYE USAILI

 • SERIKALI INAENDELEA NA JUHUDI ZA KUJENGA SEKTA YA BARABARA NCHINI

  Uboreshaji wa barabara katika kiwango cha lami katika nchi hupunguza kwa kiasi kikubwa umbali wa safari na gharama za vipuri  vya magari,  huchangia katika maendeleo ya kilimo na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje katika maeneo  ujenzi wa barabara  ulipokamilika.

 • MZANI WA KIMOKOUWA SULUHISHO LA UHARIBIFU WA BARABARA YA ARUSHA - NAMANGA

  MZANI WA KUPIMA MAGARI KIMOKOUWA SULUHISHO LA UHARIBIFU WA BARABARA YA ARUSHA - NAMANGA

 • BARABARA ZA KISASA KUONGEZEKA NCHINI

  Imeelezwa kuwa ujenzi na usimamizi bora wa barabara za kisasa katika miji mikuu utachochea kukua kwa haraka kwa uchumi na kuvutia biashara za bidhaa na utalii hapa nchini.

 • WAZIRI KAMWELWE KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA BARABARA

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, anatarajiwa kufungua mkutano wa kimataifa kuhusu mapinduzi ya sekta ya usafirishaji na mabadiliko ya kiuchumi katika nchi zinazoendelea, jijini Arusha.

 • NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA TANROADS ARUSHA KUSIMAMIA MIRADI IKAMILIKE KWA WAKATI

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa amempa miezi tisa Mkandarasi Hanil-Jiangsu Joint Venture limited anaejenga barabara ya Mchepuo ya Arusha (Arusha Bypass) kukamilisha ujenzi huo.

 • SERIKALI KUWEKEZA KWENYE HANGA KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIA

  Serikali imesema kuwa itaanza kukarabati karakana (hanga) iliyopo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), ili ndege zote zilizonunuliwa ziweze kutengenezwa hapa nchini na kuwa ya mfano kwa Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.