News

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA

Dodoma, 10 Machi, 2026

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Februari 2026 iliyowasilishwa na Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega jana Mkoani Dodoma.

Akitoa taarifa kwa Kamati hiyo, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema kuwa hadi kufikia Februari 2026, Wizara imekamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 206.33 kwa kiwango cha lami.

Ameongeza kuwa Wizara pia imekamilisha miradi 76 kati ya 81 ya dharura ya ujenzi wa madaraja yaliyoharibiwa na mvua za El-Nino pamoja na Kimbunga Hidaya katika mikoa 22 nchini ambapo miradi mitano (5) iko katika hatua za mwisho za kukamilishwa.

Kwa upande wa maendeleo ya ujenzi wa mad araja, Waziri Ulega amesema miradi mbalimbali inaendelea ambapo ujenzi wa Daraja la Pangani umefikia asilimia 70, Jangwani asilimia 26, Mbambe asilimia 44, Sukuma asilimia 76, Simiyu asilimia 73, Mirumba asilimia 50 na Mitomoni asilimia 85.