News

MTAMBO WA KUKAGUA BARABARA WAWAKIVUTIO KWENYE MKUTANO WA 18 WA JTSR 

MTAMBO WA KUKAGUA BARABARA WAWAKIVUTIO KWENYE MKUTANO WA 18 WA JTSR 

Arusha, 17 Desemba, 2025

Mtambo wa kukagua barabara wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wawakivutio kwenye mkutano wa Kutathmini Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi, unaowakutanisha Serikali, wadau wa maendeleo, wadhibiti, waendeshaji na sekta binafsi uliofanyika Jijini Arusha hivi karibu.

Mhandisi wa Majenzi wa TANROADS, Maxmilian Mwapule amesema kazi za mtambo huo ni pamoja na ukaguzi wa barabara na kuweza kutambua hitilafu na uhabirifu ambao upo tabaka la juu la barabara na matabaka ya chini.

Amesema kazi nyingine ni kutambua uwepo wa maji kwenye tabaka la chini, uwepo wa miundombinu nyingine kama mabomba ya majitaka, majisafi, gesi na mitandao. Kupitia mtambo huu TANROADS inatambua ukubwa wa tatizo na hatua stahiki za kufanya.

Bw.Madilu Athuman, Mkazi wa Mianzini ameshangazwa na hatua ya TANROADS kuweza kutumia mifumo ya kidigitali katika kukagua barabara.

“Ni hatua kubwa sana kwa serikali katika kutunza miundombinu ya barabara, ambayo inapunguza gharama kubwa za matengenezo,” amesema Bw. Madilu.

Kwa upande wake Mhandisi wa miradi, Cecilia Kalangi amesema serikali kupitia TANROADS imefanya ujenzi wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa madaraja ya Tanzanite, Wami, Mfugale, Kijazi, Uhasibu, na sasa wanaendelea ujenzi wa daraja la Mto Pangani pamoja na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato.