News

WAZIRI ULEGA AKUTANA NA MTOTO MWENYE KIPAJI CHA UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA

WAZIRI ULEGA AKUTANA NA MTOTO MWENYE KIPAJI CHA UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA

Dar es Salaam

20/07/2025

Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amekutana na mtoto Ridhiwani Martin Asheri mwenye umri wa miaka 13 kutoka Kibaigwa mkoani Dodoma, mwenye kipaji cha ujenzi wa madaraja na barabara.

Waziri Ulega amekutana na mtoto huyo tarehe 20, Julai 2025 katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, na kufanya nae mazungumzo akiwa ameongozana na familia yake.

Baada ya mazungumzo hayo Waziri Ulega ameahidi kumsaidia mtoto huyo kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuwa Mhandisi mkubwa hapo baadaye.

Waziri Ulega amesema atakaa na Wizara ya Elimu kuona njia sahihi yakufanikisha kumsaidia mtoto huyu kielimu hasa kwenye taaluma ya ujenzi.

Pia Waziri Ulega amemtembeza mtoto Ridhiwani katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ili ajionea kwa macho aliyokuwa anayatengeneza akiwa nyumbani kwao kwa kuyaona kwenye televisheni.

Miongoni mwa maeneo hayo ni Daraja la Kijazi lililopo Ubungo, Daraja la Tanzanite na kituo cha treni ya mwendokasi cha John Pombe Magufuli (SGR) kilichopo Posta.