RAIS SAMIA AAGIZA DARAJA LA J.P. MAGUFULI KULINDWA, MADEREVA WACHUKUE TAHADHARI
Mwanza
19 Juni, 2025
Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha daraja la J.P Magufuli (Kigongo–Busisi) linalindwa kikamilifu, kutokana na umuhimu wake kwa Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizindua rasmi daraja hilo leo Alhamisi, Juni 19, 2025, Rais Samia amesema daraja hilo ni kiungo muhimu cha usafiri kati ya Tanzania, Uganda na nchi jirani, na hivyo linahitaji uangalizi wa hali ya juu.
Amesisitiza madereva kuzingatia tahadhari zote za kiusalama wakati wa kulitumia. Aidha, ametaja madaraja mengine tisa yaliyokamilika katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake, yakiwemo Tanzanite, Wami, Kiegea na Gerezani, huku ujenzi wa madaraja mengine ukiendelea nchi nzima.
Amesema Serikali pia imekamilisha ujenzi wa kilomita 1,365 za barabara za lami, huku kilomita 2,380 zikiendelea kujengwa, na kuagiza matengenezo mengine kufanywa kwa wakati.