MRADI WA AWAMU YA 5 YA BRT KUHUSISHA BARABARA YA MANDELA
Dodoma
26 Mei, 2025
Katika kupunguza foleni na msongamano wa magari ya abiria na mizigo inayokwenda ndani na nje ya nchi kupitia barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam, Serikali imeliambia Bunge kuwa imeiweka barabara hiyo katika mpango wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu ya tano.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum jijini Dar es Salaam, Mariam Kisangi, ambaye ametaka kujua Serikali ina mpango gani wa kupunguza msongamano katika barabara ya Mandela, hususan eneo la Temeke kwa Sokota, ambalo limekuwa na msongamano wa magari makubwa hasa nyakati za asubuhi na jioni