News

SERIKALI KUFUNGA TAA ZA BARABARANI MIKOANI NA VIJIJINI KOTE - WAZIRI ULEGA

SERIKALI KUFUNGA TAA ZA BARABARANI MIKOANI NA VIJIJINI KOTE - WAZIRI ULEGA

 

Dodoma

05 Mei, 2025

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 Serikali itaweka taa za barabarani katika kila Mkoa katika vijiji na miji takribani 200 .Waziri Ulega amesema hayo leo tarehe 05 Mei, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ametoa maelekezo ya kuwepo kwa taa za barabarani kama mojawapo ya njia za kupunguza ajali na kuokoa maisha ya watu hapa nchini, kama sehemu ya utelekezaji wa maelekezo hayo, jumla ya taa za barabarani 4,680 zimefungwa nchi nzima ikiwa ni wastani wa taa 180 kwa kila Mkoa”“Aidha, miradi yote mikubwa ya ujenzi kwa kiwango cha lami inahusisha uwekaji wa taa za barabarani, kwa mfano, barabara yote ya Mzunguko wa Nje katika jiji la Dodoma, kilometa zote 112 zitawekwa taa za barabarani”“Kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, taa za barabarani zitawekwa katika kila mkoa katika vijiji na miji takriban 200 ambapo inatarajiwa taa 5,200 katika maeneo hayo”