News

NAIBU WAZIRI MHA. KASEKENYA ATAKA UJENZI MADARAJA YA CHAKWALE NA NGUYAMI MOROGORO KUKAMILIKA

NAIBU WAZIRI MHA. KASEKENYA ATAKA UJENZI MADARAJA YA CHAKWALE NA NGUYAMI MOROGORO KUKAMILIKA Morogoro 25 Machi, 2025 Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameelekeza kwa wakandari M/s Asabhi anayejenga daraja la Chakwale mita 80 na M/s Koberg anaejenga daraja la Nguyami 100m kuhakikisha yanakamilika kwa wakati na kwa ubora uliosanifiwa. Madaraja hayo yako katika barabara ya Iyogwe- Chakwale-Ngilori (Gairo), yenye urefu wa Km 41 ambayo inaunganisha mkoa wa Tanga- Morogoro-Dodoma kwa njia fupi. "Fedha zipo hivyo hakikisheni madaraja haya yanakamilika kwa ubora uliokusudiwa ili yaweze kubeba magari makubwa na pindi barabara ya lami itakapojengwa yasifanyiwe marekebisho", amesema Mha. Kasekenya. Naibu Waziri huyo amewataka wakazi wa wilaya za Gairo mkoani Morogoro na Kilindi mkoani Tanga kuzalisha mazao mengi ili uwekezaji unaoendelea uwanufaishe kiuchumi. Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Morogoro Mha. John Mkumbo amesema watahakikisha madaraja hayo na barabara unganishi mita 500 kila upande yanakamilika kwa wakati. "Tutawasimamia wakandarasi hawa kikamilifu ili miradi hii iwiane na thamani ya fedha na hivyo kuleta tija kwa wananchi",amesema Mha. Mkumbo. Zaidi ya shilingi Bilioni 6.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa daraja la Chakwale lenye urefu wa mita 800, wakati shilingi 7.1 Bilioni zikitarajiwa kutumika katika daraja la Nguyami lenye urefu wa mita 100.