News

NAIBU KATIBU MKUU UJENZI DR. MSONDE AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA TANROADS SHINYANGA

NAIBU KATIBU MKUU UJENZI DR. MSONDE AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA TANROADS SHINYANGA

Shinyanga

07 Feb, 2025

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dr. Charles Msonde amefanya ziara ya kikazi Mkoani Shinyanga na kuongea na Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Shinyanga.

 

Naibu Katibu Mkuu alipongeza Wafanyakazi kwa kazi nzuri ya kusimamia ujenzi na matengenezo mindombinu ya Barabara, madaraja na viwanja vya ndege, ambapo amesisitiza kuwa watumishi hao wajikite katika kusimamia viwango vya ubora na udililifu katika kutekeleza majukumu ya taasisi.

 

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Samwel Mwambungu, alitoa shukrani kwa niaba ya Watumishi wote na kuongeza kuwa, maelekezo na maagizo yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu yatatekelezwa kikamilifu na kuahidi kuongeza juhudi katika kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na matengenezo ili viwango vya ubora uliokusudiwa viweze kufikiwa.