News

TANROADS MANYARA YATOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA VIVUKO VYA VYENYE TAA ZA KUONGOZEA MAGARI

TANROADS MANYARA YATOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA VIVUKO VYA VYENYE TAA ZA KUONGOZEA MAGARI

 

Manyara

25 Januari, 2025

Ofisi ya Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Manyara imeendesha zoezi la  kutoa elimu ya matumizi sahihi ya taa zakuongozea magari na watembea Kwa miguu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Sinai na Shule ya Msingi Queen Sendiga, zilizopo Wilaya ya Babati. Lengo la zoezi hilo nikuwapa uelewa wanafunzi wa  matumizi sahihi ya kifaa hicho pindi wanapovuka Barabara. Hatua hiyo itapunguza au kuzuiya  matukio ya ajali za kugongwa wanafunzi pamoja na wananchi katika eneo hilo. Zoezi la usimikaji wa taa za kuongozea magari na watembea Kwa miguu (pedestrian traffic signals) niendelevu kwenye maneno mbalimbali katika Barabara Mkuu za Dodoma- Babati- Arusha na Babati - Singida ambayo yameripotiwa matukio ya mala Kwa mala ya ajali. Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za TANROADS Manyara kuhakikisha usalama wa watumiaji wa  barabara, hususni  katika maeneo yenye watu wengi wanaovuka Barabara kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.