News

MBUNGE UMMY MWALIMU AMSHUKURU RAIS DKT SAMIA KWA KUTOA TENA KIASI CHA BILIONI 4.7 UJENZI BARABARA YA TANGA-PANGANI

MBUNGE UMMY MWALIMU AMSHUKURU RAIS DKT SAMIA KWA KUTOA TENA KIASI CHA BILIONI 4.7 UJENZI BARABARA YA TANGA-PANGANI

 Tanga

03 Januari, 2025

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa tena kiasi cha shilingi bilioni 4.7 ili mkandarasi wa kampuni ya Chicco anayejega barabara ya Tanga hadi Pangani kwa kiwango cha lami aendelee na kazi baada ya kusimama muda mrefu.

Ummy aliyasema hayo leo wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega wakati alipotembelea ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani na kuwahakikishia wananchi waliojitokeza eneo la Kirare kunakojengwa daraja kwamba serikali imetoa fedha hizo ili ujenzi wa barabara hiyo uendelee.

“Mheshimiwa Waziri tufikishie salamu zetu kwa Rais, tunamshukuru sana kwa kutoa fedha hizi ambazo zitamfanya mkandarasi kurejea kazini na kazi ya ujenzi wa barabara hii utaendelea,” alisema Ummy.

Ummy alisema kukamilika kwa barabara ya Tanga Pangani kutainua uchumi wa wilaya hizo na manufaa yake ni makubwa na wanaamini ujio wa Waziri Ulega hauwezi kumuagusha Rais hiyo ujenzi huo utaenda kwa kasi ili waweze kufaidi matunda ya barabara ya Tanga-Pangani

“Lakini hili daraja la Kirare kwetu ni maarufu lilikuwa kero sana na barabara ikiishia Tanga Panga tutakuwa tunatumia dakika 30 hadi 25 kutoka Tanga hadi Pangani hivyo tufikishe salamu shukrani kwa Rais kwa kuwekeza fedha nyingi hapa kwani itainua uchumi na kufungua Tanga ikashindane na Mombasa Kenya kwa upande wa Utalii. Alisema

 

Aidha alisema kwamba barabara hiyo ni ya kimkakati na inagusa kata 8 kati ya kata 27 za Tanga mjini huku akieleza kati ya hizo moja ambayo ni ya Kirare imekuwa ikilima zao la Muhogo na hivyo kusafirishwa kwenda sokoni hivyo ujenzi utakapokamilika utaweza kuufungua mkoa wa Tanga na RC Balozi Dkt. Batilda Burian amekuwa kuimarisha utalii katika Mkoa wa Tanga.