News

UJENZI WA DARAJA LA SUKUMA UTAPUNGUZA AJALI

UJENZI WA DARAJA LA SUKUMA UTAPUNGUZA AJALI

 

Magu

21 Desemba 2024

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kuwa Ujenzi wa daraja la Sukuma utasaidia kupunguza ajali kwa kiasi kikubwa kutokana na daraja la zamani lilikuwa jembamba lenye njia moj, lakini la sasa litakuwa na njia mbili za magari.

 

Ameongeza kuwa ujenzi wa madaraja hayo ni moja ya utekelezaji wa mikakati ya Serikali ya kuboresha sekta ya miundombinu nchini ambapo daraja la Sukuma limefika asimia 24 na Simiyu limefika asilimia 35 ambayo yote yanagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100.

 

Amefafanua kuwa kukamilika kwa madaraja hayo kutarahisisha usafiri na usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kukuza na kuchochea uzalishaji katika sekta za kilimo, madini na viwanda.

 

Mha. Kasekenya yupo kwenye ziara ya Waziri Mkuu ya ukaguzi na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo ujenzi wa daraja la Sukuma na Simiyu ambayo yanagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100.