WAZIRI WA UJENZI MHE ULEGA AANZA ZIARA DAR ES SALAAM
Dar es Salaam
15 Desemba, 2024
Waziri wa Ujenzi, Mhe Abdallah Ulega (Mb) amewapongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu wanayoendelea kote nchini.
Waziri Ulega ametoa pongezi hizo tarehe 15 Desemba, 2024 wakati akizungumza na Menejimenti ya TANROADS ikiwa ni mwanzo wa ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Katika ziara yake ya siku moja Waziri Ulega atatembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa barabara za magari Yaendayo Haraka (BRT 3 Lot 1) kuanzia Mtaa wa Azikiwe, Posta ya zamani hadi Gongolamboto pamoja na mradi wa uboreshaji usalama barabarani katika mradi wa BRT 1 sehemu A kutoka Ubungo hadi Kimara na kuzungumza na wananchi.