TANROADS YAIMARISHA MATUMIZI YA HIFADHI YA BARABARA KANDA YA ZIWA
Tabora
13 Desemba,2024
Mkurugenzi wa Matengenezo wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Dkt. Christina Kayoza, amegawa vifaa vya kupima umbali wa mkongo wa mawasiliano (OTDR) unaotumiwa na kampuni za simu ndani ya hifadhi ya barabara zinazohudumiwa na TANROADS .
Vifaa hivyo vimegaiwa Mkoani Tabora katikaa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa matengenezo ya barabara kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa mwaka wa fedha 2024/25, ambacho Mha. Dkt. Kayoza alimwakilisha Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mha. Mohamed Besta.
Vifaa hivyo vimetolewa kwa Mameneja wa TANROADS mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma na Mara ili kuwasaidia katika upimaji wa umbali kwenye mkongo wa mawasiliano kwenye hifadhi ya barabara.
Uwepo wa vifaa hivyo, umeelezwa kwamba utaongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwa watumiaji wa hifadhi ya barabara hususani mikongo ya simu.