TANROADS YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU
Iringa
31 Agosti, 2024
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imetekeleza agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa alilotoa mnamo tarehe 08 Julai, 2024 la kukamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Iringa ili uanze kutumika mapema mwezi huu (Septemba) kwa lengo kufungua fursa za kiuchumi na kiutalii.
Katika kutekeleza agizo hilo, uwanja huo umekabidhiwa rasmi kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), tarehe 31 Agosti, 2024 ili uweze kutumika kwa ndege ya aina ya Bombadia Q400 kuanzia leo Septemba Mosi, 2024.
Kazi ya ujenzi ya uwanja huo wa ndege zilianza tarehe 24 Julai 2020 na kukamilika tarehe 30 Agosti 2024 kwa gharama ya shilingi Bilioni 63.742 ikiwemo gharama za fidia kwa wananchi kiasi cha shilingi Bilioni 2.917
Kazi za ujenzi zilitekelezwa na mkandarasi Sinohydro
Corporation Limited kutoka nchini China na kusimamiwa na Mhandisi Mshauri kutoka Kitengo cha ndani cha Ushauri wa Kihandisi cha TANROADS (TECU) Mkoa wa Iringa chini ya TANROADS Makao Makuu na Wizara ya Ujenzi.
Uwanja wa ndege wa Iringa umekamilika kwa kiwango cha kuanza kutumika (substantialy completed) tarehe 30 Agosti 2024 na utakuwa katika kipindi cha uangalizi kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia Septemba Mosi, 2024.