News

KITENGO CHA MAABARA TANROADS MANYARA CHAJIDHATITI  KATIKA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA WA NDANI NA NJE YA NCHI  

KITENGO CHA MAABARA TANROADS MANYARA CHAJIDHATITI  KATIKA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA WA NDANI NA NJE YA NCHI

 

Manyara

29 Agosti, 2024

Kitengo cha Maabara  ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Manyara  kinahusika na upimaji wa malighafi za ujenzi kwa ajili ya kuthibiti ubora wa shughuli za ujenzi wa barabara na majengo ambapo vipimo vinavyofanywa ni pamoja na kupima udongo; uimara wa zege; uimara wa matofali; ubora wa mchanga na kokoto.

Kazi za upimaji hufanyika katika maabara ya TANROADS Mkoa wa Manyara iliyosajiliwa na Bodi ya Wahandisi Tanzania (ERB) kwa usajili namba 016.

Kitengo hiki kina jukumu la kuhudumia wateja wa ndani ambao ni wakandarasi wanaotekeleza miradi ya matengenezo ya miundombinu ya barabara pamoja na madaraja na miradi ya maendeleo ambayo inasimamiwa na Ofisi ya Meneja TANROADS Mkoa wa Manyara.

Pamoja na hayo, kitengo hiki kinatoa huduma kwa wateja wa nje ikiwa ni pamoja na upimaji wa malighafi za ujenzi wa miradi inayotekelezwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara pamoja na taasisi za serikali kama TARURA, RUWASA, halmashauri pamoja na majengo ya watu binafsi.



Huduma hizo za upimaji wa malighafi za ujenzi zinatolewa kwa kufuata mwongozo wa Mkataba wa Huduma Kwa Mteja (Client Service Charter) ili kuhakikisha Wateja wanapatiwa huduma bora na kwa wakati.

 

Kitengo cha Maabara ya TANROADS Mkoa wa Manyara kina maafisa mbalimbali wanaosimamia na kutekeleza majukumu ya kazi za upimaji wa malighafi za ujenzi katika ubora unaotakiwa kwa mujibu wa miongozo ya Kihandisi (Materials Manuals and Specifications)