News

WATAALAM WA MAZINGIRA WA TANROADS WAFANYA TATHMINI YA MIRADI YA UJENZI WILAYANI SIMANJIRO

 

WATAALAM WA MAZINGIRA WA TANROADS WAFANYA TATHMINI YA MIRADI YA UJENZI WILAYANI SIMANJIRO

 

Simanjiro

15 Agosti, 2024

Wataalam wa mazingira wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Manyara na wa Makao Makuu wanaendelea na tathmini ya mazingira katika miradi ya miundombinu inayojengwa mkoani hapo.


Timu hiyo, imetembelea wilaya ya Simanjiro tarehe 15 Agosti, 2024, ambapo wamekutana na, Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Simanjiro ambaye ameishukuru ofisi ya TANROADS Mkoa wa Manyara kwa kazi nzuri ya uboreshaji wa miundombinu wanaoendelea kuifanya katika wilaya hiyo, na ameahidi kutoa ushirikiano pindi miradi ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara na madaraja itakapoanza kujengwa.


Vilevile wataalamu hao wametembelea eneo la Losinyai ambako TANROADS Mkoa wa Manyara inatarajia kujenga daraja.


Aidha, wataalamu hao wameweza kukutana na wananchi wa Kijiji cha Losinyai ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni, ushauri na mapendekezo yanayohusiana na ujenzi wa daraja katika eneo hilo.


Kwa upande wao, wananchi wa kijiji Cha Losinyai wamependekeza kwamba, pindi ujenzi wa daraja eneo la Losinyai utakapoanza wazingatiwe upanuzi sehemu ya kupitishia maji katika daraja hilo, ili kusaidia maji kupita kiurahisi bila kuathiri miundombinu ya daraja hilo.