News

TANROADS YASHIRIKI KIKAMILIFU CRDB MARATHON 2024

TANROADS YASHIRIKI KIKAMILIFU CRDB MARATHON 2024

 

Dar es Salaam

18 Agosti,2024

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) leo Jumapili Agosti 18, 2024 imeshiriki mbio za CRDB Marathon ambazo zimejielekeza kusaidia jitihada za Serikali kuboresha sekta ya afya, kusaidia wenye uhitaji pamoja na kukuza ustawi wa jamii.



Katika mbio hizo, wafanyakazi wa TANROADS wameshiriki mbio za Kilometa tano, 10 na 21.



Akizungumza mara baaada ya kushiriki mbio hizo, Mhandisi Clever Akilimali ambaye ni Msimamizi wa Idara ya Mipango wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam amesema, mbali na kushiriki mbio hizo, pia wamekuwa na desturi  ya kufanya mazoezi binafsi kwa lengo la kuimarisha afya lakini pia kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kufanya mazoezi ili kuwa na afya njema.



Mha, Akilimali amesema kuwa, wafanyakazi wa TANROADS zaidi ya 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini wameshiriki katika mbio hizo.



Naye Msimamizi wa Kitengo cha Fedha na Utawala TANROADS, mkoa wa Dar es Salaam, Neema Mtengule ametoa wito kwa watumishi wenzake kuwa wapende kushiriki kwenye mbio mbalimbali zikiwemo za CRDB, ili kujenga afya zao.



Amezitaja faida za kushiriki kwenye mbio mbalimbali ni pamoja na kuimarisha afya, kuongeza mtandao wa kufahamiana na watu, kupata fursa ya kutangaza kazi zinazofanywa na taasisi husika.