News

TANROADS KUSHIRIKIANA NA VYUO VIKUU VYA DODOMA KATIKA UPANDAJI WA MITI

TANROADS KUSHIRIKIANA NA VYUO VIKUU VYA DODOMA KATIKA UPANDAJI WA MITI

 

Dodoma

05 Juni, 2024

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wamesema watashirikiana na vyuo vikuu vya jijini Dodoma katika zoezi la upandaji miti kwenye mradi mkubwa wa Green solution for sustainable urban unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Usimamizi wa Mazingira na Jamii wa TANROADS, Bi Zafarani Madayi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani, ambapo amesema vyuo vikuu hivyo vitatumika kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo athari zilizopo kwenye mkoa wa Dodoma kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kwa baadaye itatengenezwa ramani yakuonesha maeneo yaliyopo hatarini kuathirika ikiwemo tetemeko la ardhi na mafuriko.

Bi. Madayi amesema katika mradi huo ambao unaratibiwa na TANROADS utakuwa na vipengele vikubwa vinne ambayo ni kuboresha sera na mifumo ikiwa ni kuhakikisha kwamba mabadiliko ya tabianchi yanahusishwa katika sera na mifumo mbalimbali katika taasisi, pia kutakuwa na mpango wa urejeshwaji na kusimamia maeneo yaliyoharibiwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi na shughuli za maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa barabara na madaraja, ambapo katika kipengele hiki ndipo penye zoezi la upandaji miti 18000 katika hekari 1123 kwenye mradi wa barabara za mzunguko za Dodoma na Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato.

Amesema mambo mengine ni kusimamia masuala ya uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi kwa kusaidiana na taasisi mbalimbali, na kipengele cha nne ni kukuza weledi kwa kutoa elimu na kuwajengea uwezo wa masuala ya mazingira kutoka taasisi moja na kwenda nyingine.

“Mradi huu hatuutekelezi peke yetu kama TANROADS lakini tunawadau wengine tutakaoshirikiana nao kama vile TMA wakaotusaidia taarifa za awali za hali ya hewa kama masuala ya mvua na mengine, DUWASA katika masuala ya urejeshwaji wa maji machafu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma na TSF.

Mradi huu utatekelezwa ndani ya miezi 42 kuanzia Juni 2024 na unatarajiwa kumalizika