News

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI VISHOKA WANAOSHIKILIA MAENEO YENYE MALIGHAFI ZA UJENZI

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI VISHOKA WANAOSHIKILIA MAENEO YENYE MALIGHAFI ZA UJENZI

Dodoma

29 Mei, 2024

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kujihusisha na mchezo mchafu wa kushikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi.

 

Bashungwa ameyasema hayo wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, Bungeni jijini Dodoma leo, Mei 29, 2024

 

Amesema changamoto kubwa ni uwepo wa vishoka wanaoshikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi na kutoza fedha nyingi.

 

Bashungwa amesema Wizara ya Ujenzi inaendelea na mazungumzo na Wizara ya Madini kuhusu upatikanaji wa malighafi za ujenzi ikiwemo changarawe, mchanga na kokoto.

 

“Mazungumzo hayo yanalenga kupata namna bora ya kutatua changamoto kubwa ya upatikanaji wa malighafi hizo.” amesema Bashungwa

 

“Dhamira ya Wizara ni kuwa kwa kadri inavyowezekana maeneo hayo yamilikishwe kiwa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), ili kuwezesha miradi mingi ya barabara kutekelezwa kwa wakati, na kupunguza gharama za ujenzi.”

 

Amesema upatikanaji wa malighafi za ujenzi kwa gharama nafuu itawezekana endapo  TANROADS itakuwa na maeneo ya kuchimba malighafi hizo.