KAZI ZA USIMAMIZI WA MAZINGIRA NA JAMII ZINAZOFANYWA NA TANROADS KUPITIA KURUGENZI YA MIPANGO YA MIUNDOMBINU:
SEHEMU YA MAZINGIRA NA JAMII
Dar es Salaam
20 Mei, 2024
Kuanzia mwaka 2006 Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kupitia Kurugenzi ya Mipango ya Miundombinu: Sehemu ya Mazingira na Jamii imefanikiwa kusimamia na kuratibu uandaaji na utekelezaji wa Tathmini za Athari ya Mazingira na Jamii na Mipango ya usimamizi wa Mazingira na Jamii (Environmental and Social Management Plans (ESMP) kwa miradi 150 ya Barabara, Madaraja na Viwanja vya Ndege. Mpaka sasa Wakala imefanikiwa kupata vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 82 ambapo ujenzi kwa baadhi ya miradi hiyo umekamilika; na mingine ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.
Mpaka kipindi cha Mwaka wa Fedha 2022/2023, pamoja na mambo mengine, Sehemu ya Mazingira na Jamii imeweza kufanikisha masuala yafuatayo:
- Kuandaa Sera za Taasisi katika kusimamia utekelezaji wa masuala ya Mazingira na Jamii zifuatazo:
- Sera ya UKIMWI Mahali pa Kazi ya TANROADS (TANROADS HIV and AIDS at Work Place Policy, 2015);
- Sera ya Mazingira na Jamii ya TANROADS (TANROADS Environmental and Social Management Policy, 2018); na
- Sera ya Jinsia ya TANROADS (TANROADS’ Gender Policy, 2023).
- Kuandaa Rasimu za Miongozo ya Taasisi katika kusimamia utekelezaji wa masuala ya Mazingira na Jamii kwenye miradi ya Barabara. Miongozo hiyo ambayo inategemea kukamilika katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 ni pamoja na:
- Mwongozo wa Masuala ya Mazingira na Jamii ya TANROADS (TANROADS Environmental and Social Consideration Guidelines, 2023);
- Mwongozo wa Uhamishaji wa Makazi na Ulipaji wa Fidia ya TANROADS (TANROADS Compensation and Resettlement Guideline) wa mwaka 2023;
- Mwongozo wa Ushirikishaji Wadau ya TANROADS (TANROADS Stakeholders Engagement and Participation Guidelines, 2023);
- Mwongozo wa Usuluhishi wa Malalamiko ya TANROADS (Grievance Redress Committees Guidelines).
- Uhamasishaji na Uundaji wa Kamati za Usuluhishi wa Malalamiko (Grievance Redress Committees) wakati wa utekelezaji wa miradi ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege wakati wa ulipaji fidia na ujenzi wa barabara. Kamati hizi ni mahususi kwa ajili ya kutatua migogoro mbalimbali inayotokana na utekelezaji wa miradi kuanzia wakati wa ulipaji wa fidia kwa waathiriwa wa mradi; na kutatua migogoro mbalimbali inayojitokeza wakati wa ujenzi baina ya Makandarasi na Wafanyakazi wao; Makandarasi, Wafanyakazi na Jamii inayozunguka eneo la mradi.
Kamati za usuluhishi wa malalamiko zinatumia njia ya uwazi katika kutatua malalamiko yanayojitokeza. Kamati hizi zinaundwa kwa kufuata Mwongozo wa kushughulikia masuala ya Fidia na Uhamishaji wa Makazi ya Watu uliotolewa na Wizara ya Ujenzi mwaka 2009, pamoja na miongozo ya Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Mpaka sasa Kamati hizo zimeundwa katika miradi ifuatayo:
- Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Lake Manyara;
- Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo kwa haraka Awamu ya 3;
- Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Tanga;
- Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Iringa;
- Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko wa Jiji la Dodoma (Dodoma City Outer Ring Road) (km 112.3);
- Ujenzi wa Barabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu (km 260);
- Ujenzi wa Barabara ya Mnivata – Newala – Masasi (km 160);
- Ujenzi wa Barabara ya Iringa - Kilolo (km 33);
- Ujenzi wa Barabara ya Mkange - Tungamaa – Pangani (km 160) ;
- Ujenzi wa Barabara Arusha – Holili – Taveta and Arusha Bypass (km 40);
- Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato;
- Ujenzi wa Barabara ya Dodoma (Mayamaya) – Babati (Bonga) (km 188);
- Ujenzi wa Barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 360);
- Ujenzi wa Barabara ya Iringa – Dodoma (km 260);
- Ujenzi wa Barabara ya Mafinga – Igawa (km 130);
- Ujenzi wa Ubungo – Interchange (Kijazi Flyover).
- Kuandaa Mipango na Miongozo mbalimbali ya utekelezaji na usimamizi wa masuala ya Mazingira na Jamii kwenye miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ikiwemo:
- Mwongozo wa Kusimamia Masuala ya Mazingira na Jamii (Environmental and Social Management Framework (ESMF);
- Mwongozo wa Kusimamia Ulipaji wa Fidia (Resettlement Policy Framework (RPF);
- Mpango wa Ushirikishaji wa Wadau (Stakeholder Engagement Plan (SEP)
- Mpango wa Kuzingatia Makundi Maalum (Vulnerable Groups Policy Framework (VGPF);
- Mwongozo wa Kurekebisha Malalamiko (Grievance Redress Mechanism (GRM);
- Mpango wa Usimamizi wa Kelele katika uendeshaji Viwanja vya Ndege (Noise Management Plan (NMP);
- Mpango wa Usimamizi wa Bioanuai (Biodiversity Management Plan (BMP)
- Mpango wa Usimamizi wa Urithi wa Utamaduni (Cultural Heritage Management plan (CHMP);
- Mpango wa Urejeshaji wa Maisha (Livelihood Restoration Plan (LRP);
- Mpango wa Usimamizi wa Waajiriwa (Labour Management Plan (LMP)
- Mpango Kazi wa kudhibiti Unyanyasaji wa Kijinsia (Gender Based Violence - Action Plan (GBV-AP).
- Miongozo na mipango hii iliandaliwa ili kukidhi masharti ya upatikanaji wa mikopo ya maendeleo kutoka kwa wafadhili ikiwemo Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Uandaaji wa Miongozo na Mipango hiyo umefanikisha Serikali kupitia TANROADS kupata fedha za kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya kimkakati kupitia Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika ikijumuisha miradi ifuatayo:
- Mradi wa Road to Inclusion Social Economic (RISE) unaohusisha miradi ya: Barabara ya Iringa – Kilolo (km 33.3) Mkoani Iringa; Barabara ya Mkata – Kwamsisi (km 30) Mkoani Tanga; Barabara ya Namichiga – Rwangwa (km 25) Mkoani Lindi; Barabara ya Geita – Nyikonga - Kashelo - Ilolangalu (km 25) na Ushirombo – Nanda (km 16) Mkoani Geita;
- Mradi wa Tanzania Transport Integration Project (TANTIP) unaohusisha miradi ya: Barabara ya Iringa – Msembe (km 104) Mkoani Iringa; Barabara ya Mtwara – Mingoyo – Masasi (km 200) Mkoani Mtwara; Barabara ya Lutukira - Songea (km 116) Mkoani Songea; Barabara ya Lusahunga - Rusumo (km 92) Mkoani Kagera; na
Iringa Airport Mkoani Iringa; Lake Manyara Airport Mkoani Arusha; Tanga Airport Mkoani Tanga;
- Dar es Salaam Urban Project (DUTP) unaohusisha miradi ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka (BRT) kwa awamu 1, 3 na 4;
- Mradi wa Njia ya Mabasi yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya 5;
- Mradi wa Dodoma Integrated Sustainable Transport (DIST) ambao unahusisha Barabara za Dodoma - Singida (km 50); Dodoma - Arusha (km 50); Dodoma – Morogoro (km 50); na Dodoma – Iringa (km 50);
- Ujenzi wa Barabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu (km 260);
- Ujenzi wa Barabara ya Mnivata – Newala – Masasi (km 160);
- Ujenzi wa kiwanja cha Ndege Tanga; na
- Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko wa Jiji la Dodoma (Dodoma City Outer Ring Road) (km 112.3);
- Ujenzi wa Barabara ya Mangaka – Mtambaswala – Tunduru.
- Utoaji wa Mafunzo kwa Watumishi wa TANROADS na Uhamasishaji na Uelimishaji wa Umma kuhusiana na utunzaji na usimamizi wa Mazingira katika miradi ya Barabara, Madaraja na Viwanja vya Ndege.
ORODHA YA MIRADI 82 YA BARABARA, MADARAJA NA VIWANJA VYA NDEGE ILIYOPATA VYETI VYA TATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA NA JAMII (ENVIRONMENTAL CERTIFICATES) KWA AJILI YA UTEKELEZAJI KUANZIA MWAKA 2009 – 2024
S/N |
NAME OF PROJECT |
CERTIFICATE REGISTRATION NUMBER |
DATE ISSUED |
1 |
REHABILITATION AND UPGRADING OF TANGA AIRPORT |
EC/EIA/2023/0058 |
11/11/2023 |
2 |
MTWARA-MBAMBA BAY ROAD |
EC/EIS//035 |
16/03/2017 |
3 |
UPGRADING OF GEITA-USAGARA,SENGEREMA DISTRICT-MWANZA |
EC/EIS/172 |
17/9/2009 |
4 |
MULTNATIONAL ARUSHA – NAMANGA – ATHI RIVER ROAD |
EC/EIS/24 |
8/11/2006 |
5 |
REHJABILITATION OF KOROGWE-MKUMBARA-SAME (171KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/38 |
17/9/2009 |
6 |
JANGWANI BUS DEPOT |
EC/EIS//416 |
30/6/2009 |
7 |
UPGRADING OF KIGOMA-KIDAHWE-UVINZA-ILUNDE AREA IN KIGOMA TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/141 |
5/8/2009 |
8 |
UPGRADING OF TANGA-HOROHORO ROAD (65KM) |
EC/EIS/161 |
28/8/2009 |
9 |
NEW BAGAMOYO ROAD(17KM ) WIDENING PROJECT,DAR ES SALAAM REGION ,MOROCCO TO TEGETA |
EC/EIS/210 |
15/1/2010 |
10 |
REHABILITATION AND UPGRADING OF TABORA AIRPORT |
EC/EIA/219 |
7/7/2017 |
11 |
REHABILITATION AND UPGRADING OF KIGOMA AIR PORT |
EC/EIA/220 |
7/7/2017 |
12 |
UPGRADING OF TUNDUMA-SUMBAWANGA ROAD 224.5KM (TUNDUMA-LAELA SECTION (128KM) AND LAELA-SUMBAWANGA SECTION (96.5KM),TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/285 |
28/6/2010 |
13 |
IMPROVEMENT OF NYANGUGE-MUSOMA (184.5KM) AND USAGARA-KISESA ROAD (17.5KM) PROJECT,MWANZA AND MARA REFION |
EC/EIS/312 |
14/10/2010 |
14 |
PROPOSED UPGRADING OF SUMBAWANGA-NAMANYERE-MPANDA (245KM) ROAD TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/248 |
6/8/2010 |
15 |
PROPOSED UPGRADING KALIUA-MALAGARASI-ILUNDE ROAD(156KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/313 |
3/9/2010 |
16 |
UPGRADING OF KAGOMA-LUSAHUNGA ROAD (154KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/346 |
27/1/2011 |
17 |
UPGRADING OF TABORA –URAMBO-KALIUA ROAD (126KM) TRO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/483 |
11/11/2011 |
18 |
UPGRADING OF SUMBAWANGA-MATAI-KASANGA ROAD(112KM) TO BITUMN STANDARD |
EC/EIS/452 |
24/9/2011 |
19 |
UPGRADING OF KIDAHWE-KASULU-KIBONDO NYAKANAZI ROAD (310KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/529 |
17/2/2012 |
20 |
UPGRADING OF KYAKA TO BUGENE ROAD (58KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/712 |
17/12/2012 |
21 |
REHABILITATION OF MAFINGA TO INGAWA ROAD (142KM) |
EC/EIS/728 |
13/11/2012 |
22 |
UPGRADING OF LOLIONDO-MTO WA MBU ROAD(213KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/711 |
12/10/2012 |
23 |
UPGRADING OFMAYAMAYA-BONGA ROAD(188.15KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/670 |
21/8/2012 |
24 |
UPGRADING OF MAFIA ACCESS ROAD TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/642 |
21/8/2012 |
25 |
UPGRADING OF MANGAKA –NANYUMBU-MTAMBASWALA ROAD(65.5KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/636 |
25/7/2012 |
26 |
CONSTRUCTION OF RUSUMO INTERNATIONAL BRIDGE AND ONE STOP BORDER POST FACILITATES (THE BORDER OF RWANDA AND TANZANIA IN NGARA DISTRICT,KAGERA REGION) |
EC/EIS/540 |
13/3/2012 |
27 |
CONTRUCTION OF WEIGHBRIDGE STATION |
EC/EIS/565 |
23/4/2012 |
28 |
DEVELOPMENT OF ONE-STOP BORDER POST (BOARDER OF TANZANIA AND BURUNDI) |
EC/EIS/746 |
17/12/2012 |
29 |
UPGRADING OF TABORA-NYAHUA-CHANYA ROAD TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/811 |
25/2/2013 |
30 |
WIDENING OF GEREZANI -BENDERA TATU TO KAMATA JUNCTION ROAD |
EC/EIS/647 |
24/1/2013 |
31 |
CONTRUCTION OF MALAGARASI BRIDGE AND UPGRADING OF APPROACH ROAD (48KM) |
EC/EIS/809 |
15/3/2013 |
32 |
IMPROVEMENT OF TAZARA INTERSECTION |
EC/EIS/961 |
26/7/2013 |
33 |
UPGRADING OF MAKONGOROSI-RUNGWA-ITIGI-MKIWA ROAD (413KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/941 |
26/7/2013 |
34 |
REHABILITATION AND UPGRADING OF MWANZA AIRPORT |
EC/EIA/986 |
9/07/2017 |
35 |
CONTRUCTION OF WEIGHBRIDGE AND OFFICES ALONG MAKUTANO-SIRARI ROAD |
EC/EIS/1117 |
6/10/2013 |
36 |
CONTRUCTION OF TWO WEIGHBRIDGES AND OFFICES ALONG TANGA-HOROHORO ROAD |
EC/EIS/1113 |
23/10/2013 |
37 |
REHABILIATION AND UPGRADING OF SUMBAWANGA AIRPORT |
EC/EIS/1308 |
7//2017 |
38 |
IMPROVEMENT OF ARUSHA-HOLILI(140KM) ROAD IN ARUSHA AND KILIMANJARO REGIONS AND CONSTRUCTION OF 42.41KM BYPASS ROAD TO BITUMEN STANDARD IN ARUSHA MUNICIPALITY,IN ARUSHA REGION |
EC/EIS/1434 |
30/9/2014 |
39 |
UPGRADING OF TABORA-KOGA-MPANDA IN TABORA AND KATAVI REGIONS TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/1878 |
12/6/2015 |
40 |
CONTRUCTION OF DUTHUMI BRIDGE AND ITS APPROACH ROADS |
EC/EIS/1804 |
17/4/2015 |
41 |
REHABILITATION OF LUSAHUNGA-RUSUMO (92KM)AND NYAKASANZA KOBERO(59.149KM) |
EC/EIA/2690 |
25/10/2016 |
42 |
REHABILITATION OF SAME-HIMO-MARANGU (99.73KM) |
EC/EIA/2680 |
10/10/2016 |
43 |
REHABILITATION OF MOMBO-LUSHOTO (32KM) |
EC/EIA/2681 |
10/10/2016 |
44 |
REHABILITATION OF MAKAMBAKO-SONGEA ROAD (295) |
EC/EIA/2830 |
22/12/2016 |
45 |
REHABILITATION OF MTWARA-MINGOYO-MASASI ROAD (200KM) |
EC/EIA/2833 |
22/12/2016 |
46 |
CONSTRUCTION OF TERIMNAL III AND ITS ASSOCIATED FAACILITIES AT JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT |
EC/EIA/976 |
7/07/2017 |
47 |
UPGRADING OF IRINGA-DODOMA ROAD (260KM) PROJECT |
EC/EIA/201 |
7/7/2017 |
48 |
REHABILIATION AND UPGRADING OF SHINYANGA AIRPORT |
EC/EIS/1307 |
7/7/2017 |
49 |
REHABILITATION AND UPGRADING OF MTWARA AIRPORT |
EC/EIA/2851 |
25/09/2017 |
50 |
BUS RAPID TRANSIT SYSTEM AND ASSOCIATED FACILITIES PHASE 2 (19.3 KM) AND PHASE 3 (3.6KM) PROJECTS |
EC/EIA/2018/0183 |
30/5/2018 |
51 |
DEVELOPMENT OF NEW SELANDER BRIDGE (1.03KM) AND ITS CONNECTING ROADS |
EC/EIA/2018/0058 |
13/7/2018 |
52 |
ESTABLISHMENT OF DODOMA SPORTS COMPLEX |
EC/EIA/2018/0423 |
1/8/2018 |
53 |
UPGRADING OF TEGETA-BAGAMOYO –MAKOFIA ROAD (46.9KM)AND MBEGANIPORT ACCESS ROAD (4.6KM) |
EC/EIS/2018/0419 |
29/8/2018 |
54 |
UPGRADING OF UBENA ZOMOZI-NGERENGERE (KIZUKA)SECTION (11.6KM) |
EC/EIA/2018/0432 |
7/9/2018 |
55 |
UPGRADING OF IPOLE- RUNGWA ROAD (172KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/2018/05474 |
4/12/2018 |
56 |
ESTABLISHMENT OF ONE STOP INSPECTION STATION (OSIS) FACILITIES,MUHALALA VILLAGE. |
EC/EIA/20189/0592 |
4/12/2018 |
57 |
UPGRADING OF BUGENE-KASULO ROAD(122KM) BITUMEN STANDARD |
EC/EIS/2018/0573 |
28/12/2018 |
58 |
UPGRADING OF KAMANGA-KATUNGURU-SENGEREMA ROAD (36KM)TO DOUBLE SURFACE DRESSING |
EC/EIS/2019/0197 |
21/3/2019 |
59 |
ESTABLISHMENT OF ONE STOP INSPECTION STATION ALONG THE DAR ES SALAAM CORRIDOR, VIGWAZA VILLAGE |
EC/EIA/2018/0209 |
21/3/2019 |
60 |
ESTABLISHMENT OF DODOMA CITY OUTER RING ROAD(110.2KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2019/0731 |
31/12/2019 |
61 |
UPGRADING OF KASULU-MANYOVU ROAD AND ITS BYPASS ROADS (81.6KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2018/0127 |
11/2/2019 |
62 |
UPGRADING OF TANGA –PANGANI-SAADANI-MAKURUNGE(229KM) ROAD TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2019/0287 |
27/5/2019 |
63 |
UPGRADING OF SONI-BUMBULI ROAD (21.7KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2019/0438 |
13/8/2019 |
64 |
UPGRADING OF NYAMWAGE-UTETE ROAD(33.7KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2019/0730 |
31/12/2019 |
65 |
UPGRADING OF MAKOFIA-MLANDIZI (35KM) TO FOUR LANES,DUAL CARRIAGE WAY, BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2020/0086 |
10/3/2020 |
66 |
ESTABLISHMENT OF ONE STOP BORDER POST (OSBP)SONGWE/KASUMULU-TANZANIA/MALAWI BORDER CROSSING |
EC/EIA/2020/0277 |
18/5/2020 |
67 |
UPGRADING OF OMUGAKORONGO-KIGARAMA-MURONGO ROAD (111KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2020/0563 |
13/10/2020 |
68 |
UPGRADING OF ARUSHA-KIBAYA-KONGWA ROAD(493KM) |
EC/EIS/2021/0750 |
15/11/2021 |
69 |
UPGRADING OF IRINGA-MSEMBE ROAD (104KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2021/0346 |
17/5/2021 |
70 |
UPGRADE OF DOUBLE SURFACE DRESSING OF MONDULI-ENGARUKA(NGARASH-ENGUIKI SECTION 11KM) |
EC/EIA/2021/0292 |
11/3/2021 |
71 |
DEVELOPMENT OF KIGONGO - BUSISI BRIDGE (3,200M) AND ITS 1.54KM LANE APPROACH ROADS |
EC/EIA/2021/0301 |
11/3/2021 |
72 |
UPGRADING OF KIBONDO-MABAMBA ROAD (45KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2021/0302 |
11/3/2021 |
73 |
UPGRADING OF MTWARA(MNIVATA)-NANYAMBA-TANDAHIMBA-NEWALA-MASASI ROAD (160KM) TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2021/0457 |
13/5/2021 |
74 |
UPGRADING OF NYAKAHURA-KUMUMBUGA-MURUSAGANBA-GAHUMO(34KM)KUMUMBUGA-RULENGE-MURUGARAMA(75KM)& RULENGE-KIBANGA NICKEL(32KM)TO BITUMEN STANDARD |
EC/EIA/2022/022 |
20/01/2022 |
75 |
REHABILITATION OF IGAWA-UYOLE-SONGWE-TUNDUMA(218KM) AND CONSTRUCTION OF UYOLE-SONGWE BYPASS ROAD(48.9KM) |
EC/EIA/2022/0050 |
28/02/2022 |
76 |
UPGRADING OF KYERWA – OMURUSHAKA (50 KM) ROAD |
EC/EIA/2021/8213 |
15/12/2022 |
77 |
ESTABLISHMENT OF NEW WAMI BRIDGE (510 M) AND ASSOCIATED APPROACH ROADS (3.8 KM) ALONG CHALINZE - SEGERA ROAD |
EC/EIA/2023/0003 |
02/03/2023 |
78 |
ESTABLISHMENT OF STONE QUARRY SITE,AGGREGATES PRODUCTION PLANT AND CONCRETE BATCHING PLANT AT MADOBOLE, NJOMBE REGION |
EC/EIA/2002/0008 |
03/07/2023 |
79 |
UPGRADING OF MIANZINI – OLEMRINGARINGA JUU AND OLE MRINGARINGA SUMBASHI/ TIMBORO ROAD (18KM) TO BITMEN STANDARD IN ARUSHA |
EC/EIA/2020/0583 |
26/08/2020 |
80 |
DEVELOPMENT ODF BRT STYSTEM PHASE -4 |
EC/EIA/2021/9377 |
19/8/2023 |
81 |
REHABILITATION AND UPGRADING OF MANYARA AIRPORT |
EC/EIA/2023/0057 |
11/11/2023 |
82 |
UPGRADING OF MAJIMOTO – INYONGA ROAD 152 KM TO BITUMEN STANDARDS |
EC/EIA/2023/0060 |
02/10/2023 |
Ndugu Mwananchi, ili kupata taarifa zaidi juu ya mafanikio haya unaweza kutembelea tovuti yetu ya TANROADS: www.tanroads.go.tz; Au Ofisi zetu za TANROADS za Mikoa; Au Makao Makuu ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje, Ghorofa ya 3, S.L.P 11364,10 Shaaban Robert Road/Garden Avenue Junction, Dar es Salaam. Barua Pepe: tanroadshq@tanroads.go.tz