News

NAIBU KATIBU MKUU UJENZI AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI DODOMA

NAIBU KATIBU MKUU UJENZI AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI DODOMA

 

Dodoma

16 Mei, 2024

Naibu katibu Mkuu Ujenzi Ludovick J. Nduhiye amefanya ziara ya ya kikazi Jijini Dodoma ambapo amekagua na kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Kitaifa na ile iliyoko chini ya Mkoa.

Katika ziara hiyo iliyofanyika leo tarehe 16 Mei 2024, Naibu Katibu Mkuu huyo amtembelea mradi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Msalato na kukagua maendeleo ya mradi katika eneo la njia ya kuruka na kutua ndege (runway), jengo la abiria na mnara wa kuongozea ndege ambako kazi mbalimbali zinaendelea kufanyika.

Pia amekagua kazi za matengenezo zinazoendelea katika barabara kuu ya Dodoma - Mtera na za dharura katika daraja la Matumbulu lililoko kwenye barabara hiyo ambalo liliathiriwa na mvua za El-nino.

Aidha ametembelea mradi wa barabara ya mzunguko wa nje ya jiji la Dodoma sehemu ya 2 (Lot 2) ambapo amekagua kazi za madaraja na tabaka la barabara linalochanganywa na Simenti (stabilized subbase layer).