News

TANROADS KUFANYA USANIFU KULINGANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

TANROADS KUFANYA USANIFU KULINGANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Zanzibar

15 Mei, 2024

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), imesema inafanya usanifu wa kina na usimamizi wa Ujenzi wa Viwanja vya ndege, Madaraja na Barabara kulingana na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika kongamano la sita la usalama wa usafiri wa anga la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lililofanyika leo tarehe 15 Mei 2024, Mkoani Magharibi Visiwani Zanzibar.

“Tunasimamia usanifu wa viwanja hivyo na kwa kadri hali ilivyo sasa, tunatakiwa kufanya usanifu kulingana na mabadiliko ya Hali ya hewa ili usanifu wetu uwe makini “amesema Besta

Mhandisi Besta, ameongeza kwa kusema kuwa Mabadiliko ya tabianchi yanatokea mara kwa mara na kazi kubwa ambayo TANROADS inafanya ni usanifu kwenye ujenzi wa viwanja vya ndege, Madaraja na barabara ili ziwe katika viwango vinavyotakiwa.

“Kama TANROADS tunawajibu wa kuendeleza na kusimamia ujenzi wa Viwanja vya ndege nchini na baada ya kuvikamilisha tunavikabidhi kwenye Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hali ilivyo sasa” amesisitiza Mha. Besta.

Kongamano la sita la usalama wa usafiri wa anga la Jumuiya ya Afrika Mashariki, lilifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambalo linafanyika kwa siku mbili tarehe 15 na 16 Mei 2024,Mkoani Magharibi Visiwani Zanzibar.