News

BARABARA YA KUINGIA BUKOBA MJINI YAFUNGWA KWA MUDA BAADA YA MAJI YA MVUA KUFURIKA JUU YA MADARAJA

BARABARA YA KUINGIA BUKOBA MJINI YAFUNGWA KWA MUDA BAADA YA MAJI YA MVUA KUFURIKA JUU YA MADARAJA

Bukoba

10 Mei, 2024

Barabara Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Kagera zimesababisha maji kufurika juu ya barabara kwenye maeneo ya madaraja ya Kanoni na Buyekeraya barabara kuu ya kuingia Bukoba mjini.

Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kagera Mha. Ntuli J. Mwaikokesya amekiambia kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa kuwa barabara hiyo imefungwa kwa muda leo tarehe 10 Mei 2024 kwa sababu za kiusalama wakati Wataalam wa Barabara wakiendelea kufuatia kwa ukaribu zaidi maeneo hayo.

Amesema kwa sasa magari yamechepushwa kupita kwenye barabara za Kashozi na Kashura hadi hapo itakapothibitishwa kamba maeneo hayo ni salama kupita magari na watumiaji wengine wa barabara.