SERIKALI YAIPA TANROADS BIL. 6.5 KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL-NINO MKOANI RUKWA
Rukwa
06 Mei, 2024
Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Mgeni Mwanga amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kukubali kutoa kiasi hicho cha fedha ambacho kimewezesha kurejesha miundombinu iliyoharibiwa.
Mhandisi Mwanga amesema hayo tarehe 6 Mei, 2024 baada ya kutembelea na kukagua miundombinu iliyoharibika ikiwa ni pamoja na Daraja la Solola lililopo barabara ya Ilemba – Kaoze ambapo barabara unganishi ilisombwa na maji na hivyo kufanya upana na kina cha mto kuongezeka.