News

SOMANGA YAANZA KUPITIKA, NGUVU YAELEKEZWA SONGAS

SOMANGA YAANZA KUPITIKA, NGUVU YAELEKEZWA SONGAS

Lindi

08 Mei, 2024

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Ujenzi na wakandarasi wamefanikiwa kurejesha mawasiliano ya barabara kwenye eneo la Somanga lililoharibiwa na mvua za El-Nino zinazoendelea kunyesha kwenye baadhi ya maeneo nchini.


Hadi kufikia asubuhi ya leo tarehe 8 Mei, 2024 kazi ya urejeshaji wa miundombinu ya barabara hiyo katika eneo la Somanga imefikia katika hatua za ukamilishaji hivyo kuruhusu magari yanayobeba mawe kupita katika eneo hilo na kuelekea kwenye maeneo mingine yaliyoathiriwa na mvua kwa ajili ya ukarabati.



Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Ujenzi, nguvu ya timu ya wataalam wa TANROADS kwa kushirikiana na wakandarasi inaelekezwa kuendelea na urejeshwaji wa miundombinu ya barabara katika eneo la Songas lililopo katika barabara kuu ya Lindi – Dar es Salaam ambalo pia lilikatika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kuambatana na kimbunga Hidaya.