UREJESHAJI WA MAWASILIANO BARABARA YA DAR - LINDI UNAENDELEA USIKU NA MCHANA
Lindi
07 Mei, 2024
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiambatana na Wataalam kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wamekagua kazi ya urejeshaji mawasiliano ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam ambayo inaendelea kufanyika usiku na mchana ili kuhakikisha huduma za usafiri na usafirijishaji zinarejea ifikapo siku ya Alhamisi tarehe 8 Mei, 2024.
Waziri Bashungwa ameweka kambi pamoja na wataalam hao wa TANROADS na makandarasi huku akisisitiza kuwa kazi ya urejeshaji wa mawasiliano inafanyika usiku na mchana ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ndani ya saa 72 alizoeleza awali.
Aidha, Waziri Bashungwa amesema TANROADS inatakiwa kuimarisha kitengo cha dharura, ili kuwa tayari kukabiliana na changamoto zozote zitakazojitokeza zenye kuathiri miundombinu ya barabara na madaraja.