TANROADS YAADHIMISHA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI KWA KISHINDO
Dar es Salaam
1 Mei, 2024
WATUMISHI wa Vitengo na Idara mbalimbali za Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wa Makao Makuu na Ofisi za Mikoa yote ya Tanzania Bara wameadhimisha sherehe za Wafanyakazi zinazofanyika kila mwaka tarehe 1 Mei, ambapo pia wamehimizwa kufanya kazi kwa bidii ili kuliletea taifa letu tija.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa TANROADS Makao Makuu, Bi. Scolastica Mgaya katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa kwenye uwanja wa Uhur, lakin kitaifa yamefanyikia Jijini Arusha, na mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango aliyemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Bi. Mgaya amesema siku hii ni muhimu kwa kuwa inaleta umoja vizuri, pia unakumbusha wajibu na kutekeleza vyema majukumu yao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma kwa lengo la kujenga taifa na sio siku ya kushinikiza viongozi.
“Hii siku ni siku muhimu sana kwa wafanyakazi kote Ulimwenguni maana mbali na kutukutanisha wote, lakini inatukumbusha wajibu wetu na utekelezaji wa majukumu yetu, na sio siku ya kuanza kushinikiza kwa viongozi wetu juu ya mambo mbalimbali, tunaona mara kwa mara Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anahimiza watumishi kufanya kazi kwa bidii” amesisitiza Bi. Mgaya.
Amesema watumishi wa TANROADS wanahakikisha wamejikita katika kutekeleza majukumu ya ujenzi wa barabara na miundombinu ya serikali, ikiwa ni pamoja na barabara ziwepo katika hali nzuri ya kupitika wakati wote na hata kufanyia marekebisho ya haraka mara zitakapoathirika na mafuriko ya mvua zikiwemo za El-Nino.
Bi. Mgaya amemshukuru Mhe. Rais kwa kufanikisha upatikanaji wa haraka wa fedha zinazotumika katika marekebisho ya miundombinu inayopata madhara.
“Kwa namna ya pekee ninamshukuru Mtendaji wetu Mkuu, Mhandisi Mohamed Besta kwa uongozi wake mahiri, amekuwa halali akihakikisha shughuli zote za taasisi zinaenda vizuri, pia tunawashukuru Wakurugenzi na Mameneja wote hawachoki wanahakikisha wanatusimamia vyema na tunawashukuru pia wafanyakazi kwa kujitoa kwao kwa kufanya kazi kwa masaa mengi kuhakikisha huduma za barabara zinakwenda na kupitika kwa wakati,”