TANROADS TANGA YAFANYA KAZI YA KUZIBA MASHIMO BARABARANI YALIYOSABABISHWA NA MVUA
Tanga
28 Aprili,2024
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tanga leo tarehe 28 Aprili 2024; imeendelea na kazi ya kukabiliana na madhara ya mafuriko ya mvua kwenye miumbombinu ya barabara ikiwa ni pamoja na kuziba mashimo makubwa yaliyojitokeza barabarani kutokana na mvua hizo.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Mha. Dastan Singano amesema kazi imefanyika mzunguko wa Korogwe, makutano ya barabara ya Handeni - Korogwe na Segera - Mkomazi.
Amesema uwepo wa mashimo hayo barabarani umechangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini, ambapo TANROADS imejipanga kufanya kazi hiyo haraka kadri inavyowezekana.