News

TANROADS KILIMANJARO YACHUKUA HATUA ZA KUZUIA MADHARA ZAIDI KATIKA DARAJA LA RAU

TANROADS KILIMANJARO YACHUKUA HATUA ZA KUZUIA MADHARA ZAIDI KATIKA DARAJA LA RAU

Moshi

25 Aprili, 2024
Wakala ya Barabara Tanzania (TANRODS) Mkoa wa Kilimanjaro imechukua hatua za haraka kuzuia athari zaidi zisijitokeze katika daraja la RAU ambalo upande wa juu umeanza kuathiriwa na mafuriko ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro, Mha. Motta Kyando amekiambia kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa leo kuwa kutokana na mvua kubwa zilizonyesha tarehe 25 Aprili 2024, zimesababisha kingo za daraja hilo upande wa juu wa mto zimeathirika.

Amesema tayari timu ya Watalaam wa TANROADS na Mkandarasi wapo kazini kuimarisha kingo hizo, ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo zinazoendelea kunyesha.

Ameeleza pamoja na kingo hizo kuathiri lakini daraja hilo lililopo Manispaa ya Moshi katika barabara ya Mkomazi West (Kilimanjaro /Tanga border) - Same - Himo Jct - KIA Jct (Kilimanjaro/Arusha border) liko salama na watumia barabara wanaendelea kulitumia kama kawaida.