MAWASILIANO YA BARABARA YA HANDENI-KIBERASHI ENEO LA MABALANGA YAJEREA
Tanga
24 Aprili,2024
Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tanga imerejesha mawasiliano ya barabara ya Handeni - Kiberashi katika kijiji cha Mabalanga baada ya kuharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Mha. Dastan Singano amesema kazi hiyo imefanyika usiku wa kuamkia jana tarehe 24 April 2024; sehemu hiyo ya barabara imeimarishwa na magari yanapita bila shida.