News

TANROADS YAKAMILISHA UJENZI WA NJIA MBADALA ENEO LA DARAJA LA MTO LOSINYAI MKOANI MANYARA LILILOHARIBIWA NA MAFURIKI YA MAJI YA MVUA

TANROADS YAKAMILISHA UJENZI WA NJIA MBADALA ENEO LA DARAJA LA MTO LOSINYAI MKOANI MANYARA LILILOHARIBIWA NA MAFURIKI YA MAJI YA MVUA

Manyara

13 April, 2024

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha ujenzi wa njia mbadala kwa ajili ya kupita magari katika kijiji cha Kastam wakati ujenzi wa daraja la mto Losinyai linalounganisha Wilaya ya Simanjiro na Mkoa ukiendelea.

Akizungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa tarehe 13 Machi 2024; Meneja wa TANROADS Mkoa wa Manyara Mha. Dutu Masele amesema daraja hilo linafanyiwa matengenezo baada kuharibiwa na maji ya mafuriko ya mvua kubwa za el-nino zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali Mkoani humo.

Amesema timu ya Watalaam wa TANROADS tayari imeondoa magogo na taka ngumu zilizoziba daraja hilo huku wakiendelea na kazi ya matengenezo ya miundombinu imara itakayowezesha daraja hilo kuendelea kutumika tena.

Amesema kwa sasa magari yanaendelea kupita katika njia mbadala ambapo pia Wananchi wameendelea na shughuli zao za uzalishaji.