News

MIAKA 3 YA DKT SAMIA ILIVYOFUNGUA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA

MIAKA 3 YA DKT SAMIA ILIVYOFUNGUA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA

TABORA

MACHI 6, 2024

Katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali ya Awamu ya Sita, chini Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, imetekeleza zaidi ya miradi 9  Mkoani Tabora ambapo katika miradi hiyo mitatu imekamilika na Sita inaendelea kutekelezwa.

 

Miradi iliyokamilika ni Barabara ya Nyahua-Chaya ( Km 85.4), Usesula-Komanga (km108.0), Komanga-Kasinde ( 108.0),  miradi ambayo ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji  ni barabara ya Kazilambwa-Chagu (km 36.5),Ipole- Rungwa (Km 0.6),Mambali-Bukene-Itobo (km 1.1), Puge- Ziba-Choma (Km 109.0),Tabora -Ulyankulu (km 90.0) na ukarabati na ujenzi wa uwanja wa ndege na jengo la abiria, Uzio wa jingo la kuongoza ndege na maegesho.

 

Hayo yamesemwa na Meneja wa Wakala wa Barabra Tanzania ( TANROADS) Mkoa wa Tabora, Mhandisi Raphael Mlimaji alipozungumza na kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa tarehe 7 Machi 2024 kuhusu utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ya barabara katika kipindi cha miaka mitatu cha Serikali ya awamu ya sita.

 

“Ndani ya Miaka 3  Tunamshukuru Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kutuboreshea miundombinu ya Barabara na madaraja na  ameshatenga fedha kwa ajili ya kumalizia utekelezaji wa miradi 6 iliyobakia katika mkoa wetu wa Tabora, ikiwepo ujenzi wa jengo la kisasa katika uwanja wetu wa ndege na pataweza kuhudumia zaidi ya abiria 120  na magari 54 kwa wakati mmoja” amesema Mhandisi Raphael

 

Amesema katika kipindi hicho miradi hiyo imewezesha kupatika ajira na vibarua  zaidi ya elf 4000, kwenye miradi ya Barabara na madaraja Mkoani humo.

 

Amesema TANROADS inahakikisha  inathibiti magari yanayozidisha uzito ili kuendelea kuzilinda Barabara zote za Mkoa huo; ambapo ametoa wito kwa  Wananchi kutunza Miundombinu ya Barabara kwa kutokufanya biashara au kulima kwenye hifadhi ya barabara kwani kufanya hivyo kunapelekea Miundombinu hiyo kuharibika na kuchakaa kwa haraka Tofauti na muda uliopangwa.

 

Pia, amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu, pamoja na Waziri wa Ujenzi, na Waziri wa Ofisi ya Rais-Tamisemi, kuweka mikakati juu ya wakandarasi Wazawa kupewa kipaumbele kwenye Ujenzi wa barabara za miradi mikubwa.

 

Kwa upande wake, Msimamizi Kitengo cha miradi ya Maendeleo TANROADS, Mhandisi Emanuel ngowi amesema mafanikio mengine ni pamoja na kuwa na mizani kubwa za kudumu tatu  na mmoja wa Mkeka.