News

Mhe. Rais Dkt Samia afanya makubwa utekelezaji wa miradi ya miundombinu Arusha

Mhe. Rais Dkt Samia afanya makubwa utekelezaji wa miradi ya miundombinu Arusha

Arusha,

Machi 01, 2024

Katika kipindi cha miaka 3 cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mafanikio makubwa yamepatikana katika Sekta ya Ujenzi kwenye maeneo ya Barabara na madaraja katika Mkoa wa Arusha.

 

Juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia TANROADS zimefanikisha matengenezo na ukarabati wa barabara na madaraja, ongezeko la bajeti ya matengenezo na kuongezeka kwa mtandao wa barabara za lami kutoka kilometa 425.78 zilizokuwepo Mwaka 2021 hadi kufikia kilometa 478.78 Mwaka 2024 ambapo ni ongezeko la kilomita 53.

Akizungumza na Waandidhi wa Habari Jijini Arusha tarehe 01 Machi 2024; Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha Mha. Reginald R. Massawe amesema barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami katika miaka mitatu ya awamu ya sita ni; Wasso-Sale kilomita 49, T/Packers-Bypass (km, 1) na Kijenge – Usariver (km, 3).

Amesema zaidi ya kilomita 152 ziko katika hatua mbali mbali za ujenzi kwa kiwango cha lami; Mianzini-Ngaramtoni Juu (km, 18), Karatu-Kilimapunda (km, 51), T/Packgers – Losinyai (km, 22), Mbaunda-Losinyai (km, 28), Mto wa Mbu-Selela (km, 23) na Wasso-Loliondo (km, 10).

Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaendelea kufanyika katika kila kona ya Mkoa wa Arusha; miradi ya barabara iliyosainiwa na iko katika hatua mbalimbali za ujenzi ni pamoja na barabara ya mto wa mbu kwenda loliondo (km, 217)

Ameeleza Serikali imeanza mchakato wa Ujenzi wa barabara Arusha-Kibaya-Kongwa (km, 453) na Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) na barabara ya Arusha - Kibaya - Kongwa yenye urefu wa kilometa 453.2.

Kuna Ujenzi wa barabara ya Ngaresh – Enguik (Monduli Juu) km 11.66 kwa kiwango cha lami ambapo Utaratibu wa kutangaza zabuni ya kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi huo uko katika hatua za mwisho.

Mha. Massawe ametaja miradi ya madaraja iliyokamilika kujengwa ni Daraja la Nduruma, Daraja la Kimosonu na katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita jumla ya taa 991 zimewekwa katika barabara za Arusha-Namanga, (285) Arusha-Minjingu (254) Kijenga-Usariver (239) Makuyuni-Ngorongoro (140), Arusha Bypass (43) na T/packers-Losinyai (30).