News

Bodi ya Ushauri ya TANROADS yakagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato

Bodi ya Ushauri ya TANROADS yakagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Msalato

 

Dar es Salaam

Februari 16, 2024

 

Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imetembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato Jijini Dodoma.

 

Akizungumza muda mfupi baada ya kufanyika kwa kikao cha Bodi kisha kukagua ujenzi wa uwanja huo leo tarehe 16 Februari, 2024, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Amin Mcharo ameeleza kuwa sehemu ya kwanza ya mradi huo unaojengwa na Mkandarasi M/s Sinohydro Corporation Ltd ambao unahusisha ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya magari, uzio na mfumo wa maji unaendelea vizuri.

 

“Kwenye mradi huu sehemu hii tumeona unaenda vizuri, upo kwenye 50% ulitakiwa uwe 54% upo nyuma kidogo lakini tumeona juhudi za Mkandarasi kwa hiyo hilo halitakuwa tatizo katika kuweza kufidia huo muda ambao umepotea,”

 

Kuhusu sehemu ya pili ya mradi huo, Mwenyekiti huyo amesema Bodi inakaa kikao kuona ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa na mkandarasi wa Kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group Co Ltd ikishirikiana na M/s Heber Construction Group Corporation Ltd, wanaohusika na ujebnzi wa jingo la abiria, mnara wa kuongozea ndege, kituo cha zimamoto na umeme.

 

Amesema licha ya TANROADS na Mhandisi Mshauri M/s Beza Consulting Engineering Plc akishirikiana na M/s Ambicon Engineering Ltd na M/s Afrisa Consulting Ltd kuweka msisitizo wa mara kwa mara kwa wakandarasi hao kuharakisha mradi huo lakini wameshindwa kuongeza juhudi zozote, hivyo bodi inafanya kikao na kuweza kushauri  hatua gani ziweze kuchukuliwa ili kuhakikisha mradi unakwenda kwa ka iliyokusudiwa.

 

Ameeleza kuwa “Sehemu hii ya pili (package 2) maendeleo ya mradi yapo nyuma sana, walitakiwa wawe kwenye 23% lakini wapo 13% hivyo wapo nyuma kwa 10% hapa tulipo ilitakiwa tuwe ghorofa ya pili lakini tupo ardhini (ground), tumeongea na Mkandarasi inaonekana uwezo wake wa kutekeleza hii kazi ni mdogo licha msimamizi wa mradi na TANROADS kuwa wanasisitiza kuhusu yeye kuongeza bidii katika utendaji wake”