News

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wapongeza ujenzi wa miundombinu Bara

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wapongeza ujenzi wa miundombinu Bara

29 Novemba, 2023

KAMATI ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, limeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita iliyopo chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga miundombinu ya Barabara na Viwanja vya Ndege kazi inayofanywa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kohani, Mhe. Yahya Rashid Abdallah ametoa pongezi hizo baada ya wajumbe wa kamati hiyo kutembelea Makao Makuu ya TANROADS na kupata maelezo mbalimbali ya utendaji wa kazi, na baadae kutembelea miradi ya daraja la Tanzanite na Barabara ya mabasi ya mwendakasi (BRT).

“Ninaishukuru serikali inayoongozwa na Mhe Mama Samia kwa jitihada kubwa inayofanya ya kuendeleza miundombinu, kwa kweli serikali inadhamira njema katika kuinua uchumi wa nchi, wananchi pamoja na ustawi kwa ujumla,” amesema Mhe. Abdallah.

Hatahivyo, amesema kutokana na ziara hii ya mafunzo wameweza kuchukua yale yaliyo mazuri na watakwenda kuishauri serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juhudi ambazo zinachukuliwa katika uendelezaji wa ujenzi wa miradi ya miundombinu ya Barabara na viwanja vya ndege.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Geofrey Kasekenya ameipongeza kamati hiyo, kwa kuja Bara kubadilishana uzoefu na kuona shughuli ambazo serikali ya awamu ya sita inazofanya. katika utendaji kazi katika miundombinu ya uchukuzi.

Hatahivyo, Mha. Kasekenya amesema kadri uchumi unavyofunguka unategemea zaidi miundombinu ya Barabara kuwa nzuri, ambapo pia zinategemewa na nchi jirani wanaotumia bandari za Tanzania Bara kusafirisha mizigo inayotoka Barani Ulaya.

“Kama tunavyojua Jijini la Dar es Salaam ndio kitovu cha biashara katika Tanzania na ndipo penye bandari kuu inayopokea nizigo kutoka nchi mbalimbali duniani na hata kutumika kwa kupeleka mizigo nchi nyingine Duniani na nchi zinazotuzunguka.”  Amesema Mha. Kasekenya.

Halikadhalika amesema mradi wa BRT utakapokamilika utasaidia sana kupunguza foleni kwa wananchi hivyo itawarahisishia kutoka kwenye maeneo yao ya nyumbani na kufika kwa haraka maeneo ya kazi nae neo la uzalishaji, na kufanya kazi kwa tija ili kukuza uchumi wa nchi.

Amesema anachokifanya Mhe. Rais Samia baada ya kuwekeza fedha nyingi ni kuhakikisha wananchi wanatumia muda muda mfupi na gharama ndogo wakati wa kwenda kwenye majukumu yao, na maeneo ya uzalisha.

Awali akitoa taarifa fupi kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Dorothy Mtenga, amesema kuwa Wakala hiyo inamajukumu ya kujenga, kukarabati miundombinu ya Barabara, madaraja na viwanja vya ndege, ambapo unasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 11,966.38, mizani za kupima uzito wa magari 76 na madaraja 3139 katika barabara kuu na zile za mikoa na ujenzi wa viwanja vya ndege saba vilivyuokamilika, na sasa viwanja tisa vinavyoendelea kujengwa