News

PRESIDENT SAMIA SULUHU HASSAN SATISFIED WITH THE PROGRESS OF J.P MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan leo tarehe 14 Juni, 2023 amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) na ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75 na barabara unganishi km 1.66.

Akizungumza na Wananchi walijitokeza kushuhudia ukaguzi huo, Rais Dkt Samia amesema daraja hilo litakapokamilika ni faida kwa Watanzania wote, kwani litaendelea kutoa ajira maisha yote na ni kituo kikubwa cha magari yanayopita eneo hilo kwenda Nchi jirani.

Amesema "Hili daraja ni kwa ajili yetu sote, niwaombe sana tutoe ushirikiano, tusiharibu miundombinu yetu, nawapongeze mpaka hapa mlipofikia ni matumaini yangu halina muda mrefu litakamilika, tuache mafundi na makandarasi wafanye kazi yao kwa uzuri ili tukabidhiwe daraja madhubuti"

Naye Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema daraja hilo ambalo linajengwa kwa gharama ya shilingi billioni 716 ni la sita katika Afrika kwa ukubwa

"Hili ni jambo kubwa Mhe. Rais tunakushukuru sana, wakati wote hakuna kilichosinama hapa mradi unaendelea kutekelezwa masaa 24 kwa siku, umetoa maelekezo hapa nikuhakikishie kwamba tunakwenda kusimamia daraja hili kuhakikisha kila kazi inayofanyika inakamilika kwa viwango vinavyokubalika kwenye mkataba" Ameongeza Waziri Pro. Mbarawa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandishi Mohamed Besta amesisitiza daraja hilo linalojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 100% litakapokamilika litarahisisha usafiri kwa majira yote ya mwaka kwa masaa 24, litamaliza msongamano wa magari uliokuwa unatokea wakati wa kutumia vivuko, kupunguza muda wa usafiri na litakuwa kichocheo cha uchumi kwa ukanda wa ziwa Victoria na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa Utekelezaji wa mradi huo ulianza tarehe 25 Februari 2020, muda wa mkataba ni miezi 48, na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika Februari 24 mwakani 2024.