News

CONSTRUCTION OF KIGOMA AIRPORT WILL INCREASE INVESTMENT IN THE REGION.

KIWANJA CHA NDEGE KIGOMA KULETA FURSA ZA UWEKEZAJI KIGOMA

Baada ya kukamilika kwa zoezi la Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Jengo la Abiria na Mnara wa Kuongozea Ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa alipata nafasi ya kuzungumzia uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Kigoma na kueleza kuwa huo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali wa kuufungua ukanda wa magharibi mwa Tanzania kwa njia ya anga.

 

Akieleza mikakati mingine ya Serikali ya Awamu ya Sita kuwa ni pamoja na kuhakikisha kiwanja cha ndege cha Tabora, Sumbawanga na Shinyanga, vinaboreshwa maji, reli na barabara akiwataka wananchi kutumia fursa hizo kukuza kilimo, biashara, utalii na huduma ili maendeleo ya miundombinu yaendane na maendeleo ya jamii kiuchumi.

 

Mhandisi Rogatus Mativila, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, akaeleza kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutakiongezea hadhi kiwanja cha ndege cha Kigoma na kuwezesha ndege nyingi kutumia kiwanja hicho.

 

Amesema ujenzi huo pia utahusisha uzio wa kiwanja na barabara za kuingia na kutoka katika kiwanja hicho ambapo Mkandarasi wa Kampuni ya China Railway Engineering Group Company Ltd kutoka China ameshinda zabuni ya kujenga kiwanja hicho kwa muda wa miezi 18 kwa gharama ya shilingi bilioni 46.68.