News

BARABARA YA MCHEPUKO WA KUSINI (ARUSHA BYPASS) ARUSHA HADI KENYA KM 42.4 YAFUNGULIWA RASMI.

Leo tarehe 21 julai 2022 kumefanyika ufunguzi rasmi wa Barabara ya mchepuo ya Arusha (Arusha Bypass) yenye urefu wa km 42.4. Uzinduzi huo uliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mwenzake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huku ukihudhuriwa pia na wakuu wa nchi na serikali wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, viongozi wa Jamhuri ya Sudan pamoja na Somalia.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa Barabara ya Kimataifa ya Arusha hadi Holili na Voi awamu ya 1 inayohusisha sehemu ya Sakina hadi Tengeru, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania, Mhandisi. Rogatus Mativila alibainisha kuwa ujenzi wa barabara ya mchepuo ya jiji la Arusha ulilenga kuruhusu magari yasiyoishia safari zake katikati ya jiji la Arusha kupita pembezoni mwa jiji ili kupunguza msongamano katikakati ya jiji hilo na mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh. Billion 197.45 hadi kukamilika kwake.

Akihutubia hadhara Rais Uhuru Kenyata alisema kuwa uwepo wa barabara hii utakuwa wa manufaa kwani utasaidia kupunguza msongamano wa magari na itaimariisha biashara kwa kurahisisha usafirishaji wa mizigo lakini pia itaendelea kuunganisha watu wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha Rais Uhuru alihitimisha kwa kutoa shukrani kwa zake kwa Benki ya Afrika (AfDB) kwa kusaidia utekelezaji wa mradi lakini pia kwa Rais Samia Suluhu kwa uchapakazi wake.

Naye Rais Samia Suluhu Hassan alipongeza na kutoa shukrani kwa wizara, TANROADS, wakandarasi, wadau wa maendeleo Mfuko wa Maendeleo ya Afrika na Shirika la maendeleo la Japan (JICA) pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kukamilika kwa mradi huu. Aliongezea kuwa barabara hii itachochea shughuli za kiuchumi katika ukanda huo ikiwemo utalii lakini pia alitoa wito juu wa utunzaji wa miundombinu ya barabara kwani inagharimu fedha nyingi.